Victoria Kimani Asema Ukimya wa Mashabiki Unakatisha Tamaa

Victoria Kimani Asema Ukimya wa Mashabiki Unakatisha Tamaa

Mwanamuziki wa Kenya, Victoria Kimani, ameibua mjadala mtandaoni baada ya kulalamikia zaidi ya watazamaji 25,000 wa Insta Story zake wanaoangalia maudhui yake bila kuonyesha ushirikiano wowote. Kupitia Instastory yake Instagram, Kimani amesema hali hiyo inamfanya ajihisi kupuuzwa licha ya watu wengi kutazama maudhui yake. Ameongeza kuwa hali ya kuwa na watazamaji wengi kimya inamfanya aone kama juhudi zake hazithaminiwi ipasavyo. Kupitia ujumbe wake, ametoa pia wito kwa mashabiki wake kuwa na ushirikiano wa karibu zaidi kwa kuonyesha mapenzi yao kupitia likes, maoni na ku-share au kushiriki maudhui yake. Mrembo huyo amesisitiza kuwa ushirikiano huo ni muhimu kwa wasanii kwa sababu huwapa motisha ya kuendelea kutoa kazi bora na kuendeleza uhusiano wa karibu na wafuasi wao.

Read More
 Victoria Kimani Akanusha Kumlenga Diamond Katika Kauli Yake ya Rolls Royce

Victoria Kimani Akanusha Kumlenga Diamond Katika Kauli Yake ya Rolls Royce

Msanii wa muziki wa R&B kutoka Kenya, Victoria Kimani, hatimaye amejibu ukosoaji ulioibuka baada ya mahojiano yake kwenye Mic Cheque Podcast, ambako alitoa kauli iliyotafsiriwa na wengi kuwa ni dongo kwa msanii nyota wa Tanzania, Diamond Platnumz. Katika mahojiano hayo, Kimani alidai kuwa kuna Rolls Royce ya rangi ya buluu inayodaiwa kuwa ya bandia, kauli ambayo iliwafanya mashabiki wengi kuamini kuwa alikuwa akimlenga Diamond, ambaye hivi majuzi alijivunia kumiliki gari hilo la kifahari. Hata hivyo, akizungumza katika mahojiano na mtangazaji Milard Ayo, Victoria Kimani alikanusha madai hayo kwa kusisitiza kuwa hakuwa amemtaja mtu yeyote kwa jina. “Sikutaja jina la mtu yeyote… acheni. Nilisema nilichosema, haikuwa maana ya ndani,” alisema Kimani kwa msisitizo. Kauli hiyo ya Kimani imeibua mjadala mkali mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimtetea kwa kusema ana uhuru wa kutoa maoni yake, na wengine wakimtaka awe makini na matamshi yake, hasa inapohusiana na wasanii wengine wakubwa wa Afrika Mashariki. Diamond Platnumz hajatoa tamko rasmi kuhusiana na madai hayo, huku baadhi ya mashabiki wake wakimtetea vikali kwenye mitandao ya kijamii. Mashabiki sasa wanasubiri kuona iwapo kutakuwa na mwendelezo wa mvutano huu au kama pande zote zitapuuza na kuendelea na kazi zao za kisanaa.

Read More
 Victoria Kimani: “Sijawahi Kutongozwa na Mwanaume wa Kenya”

Victoria Kimani: “Sijawahi Kutongozwa na Mwanaume wa Kenya”

Mwanamuziki maarufu wa Kenya, Victoria Kimani, amezua gumzo mitandaoni baada ya kudai kuwa hajawahi kutongozwa kimapenzi na mwanaume yeyote wa Kenya. Katika mahojiano ya hivi karibuni, Kimani alisema kuwa licha ya kuwa mzaliwa na mzawa wa Kenya, wanaume kutoka taifa hilo hawajawahi kumwonyesha nia ya kimapenzi, na hata wanapojaribu, lugha yao ya ushawishi huwa haina mvuto. “Wanaume wa Kenya hawajawahi kunitongoza. Na ikitokea, lugha yao ya kimapenzi haivutii kabisa,” alisema Kimani. Ameongeza kuwa mara nyingi wanaume kutoka mataifa ya nje ndio humfuata kwa mapenzi, huku akieleza kuwa tofauti ya ujasiri na mbinu zao za ushawishi ni kubwa ikilinganishwa na Wakenya. Victoria, ambaye amewahi kufanya kazi na wanamuziki wa kimataifa na kuishi katika mataifa mbalimbali, alisisitiza kuwa hana kinyongo na wanaume wa nyumbani, lakini anatamani kuona mabadiliko katika jinsi wanavyoonyesha mapenzi yao. Kauli hiyo imeibua mjadala mkali mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakimtetea huku wengine wakihisi kuwa anawadharau wanaume wa taifa lake. Wengine walihoji kuwa labda hofu ya umaarufu wake au hadhi yake ya juu ndiyo huwafanya wanaume wa Kenya kutojaribu kumtongoza. Victoria Kimani ameendelea kuwa mmoja wa wasanii wa kike wa Kenya wanaotambulika kimataifa kutokana na sauti yake ya kipekee, mitindo ya kisasa, na ujasiri wa kusema anachohisi bila woga.

Read More
 Victoria Kimani Amrushia Dongo Diamond Platnumz: Adai Rolls Royce ya Buluu Ni ya Bandia

Victoria Kimani Amrushia Dongo Diamond Platnumz: Adai Rolls Royce ya Buluu Ni ya Bandia

Mwanamuziki na mtunzi mashuhuri Victoria Kimani amezua gumzo mitandaoni baada ya kudokeza kuhusu gari la kifahari aina ya Rolls Royce linalodaiwa kuwa la bandia, ambalo linapigiwa debe katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Victoria alirusha dongo la chinichini kwa mtu mashuhuri ambaye hakumtaja moja kwa moja, akidai kuwa anajigamba na gari la kifahari lisilo halisi. “Si kila Rolls Royce ya buluu unayoiona mitaani ni halisi. Wengine wanapenda kuishi kwa kiki kuliko uhalisia,” alisema Kimani. Ingawa hakumtaja jina mhusika, mashabiki na wachambuzi wa mitandao walihisi kuwa ujumbe huo umeelekezwa kwa kwa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye hivi karibuni ameonekana mara kwa mara akipiga picha na gari la kifahari la rangi ya buluu katika hafla mbalimbali. Kauli ya Kimani imezua maoni mseto, baadhi wakimpongeza kwa kusema ukweli huku wengine wakimshutumu kwa kuanzisha mzozo usio na msingi. Wafuasi wa Diamond wamemkingia kifua msanii wao, wakisisitiza kuwa gari hilo ni halisi na lilinunuliwa kihalali. Diamond Platnumz bado hajajibu hadharani kuhusu suala hilo, lakini mijadala inaendelea kushika kasi mitandaoni huku mashabiki wakingoja kuona iwapo atatoa majibu au kulipuuza kabisa.

Read More
 Victoria Kimani: Nauli Ilinizuia Kufikia Ndoto Yangu Marekani

Victoria Kimani: Nauli Ilinizuia Kufikia Ndoto Yangu Marekani

Mwanamuziki wa Kenya anayeishi Marekani, Victoria Kimani, amefichua tukio la kusikitisha ya jinsi alivyopoteza moja ya nafasi kubwa katika taaluma yake ya muziki kwa sababu ya ukosefu wa nauli. Katika mahojiano ya hivi majuzi, Victoria alisimulia kuwa aliwahi kukutana na rapa na mjasiriamali maarufu wa Marekani, Sean Combs, maarufu kama P Diddy, wakati walipokuwa kwenye studio moja. Tukio hilo lilimfungulia mlango wa pili wa fursa kubwa, kwani alialikwa tena kwa ajili ya kufanya kazi kama vocal producer kwenye wimbo wa mwanamuziki Cassie, aliyekuwa mchumba wa Diddy kwa muda mrefu. Hata hivyo, licha ya msisimko wa mwaliko huo, Victoria alisema hakuweza kuhudhuria kipindi cha pili cha kurekodi kwa sababu hakumudu gharama ya nauli ya teksi wala treni kwenda studio.  “Niliitwa tena ili kusaidia kurekodi sauti kwa ajili ya Cassie, lakini wakati huo sikuwa na hata senti ya nauli. Sikuwa na teksi, wala hata nauli ya treni,” alieleza kwa masikitiko. Kauli hiyo imewagusa mashabiki wengi mitandaoni, wengi wakimsifia kwa ujasiri wa kushiriki hadithi ya wakati mgumu maishani mwake, huku wengine wakihuzunishwa na namna talanta inaweza kukosa kung’aa kutokana na changamoto za kifedha. Victoria Kimani amekuwa mmoja wa wasanii wa kike wa Kenya waliowahi kutambulika kimataifa, akifanya kazi na majina makubwa katika muziki wa Afrika na Marekani. Hadithi yake inasisitiza umuhimu wa msaada kwa wasanii chipukizi, hasa wanapokuwa katika hatua za mwanzo za taaluma zao.

Read More
 Victoria Kimani Abadilika Kimtindo, Asema Atafunguka Zaidi Kwenye Documentary

Victoria Kimani Abadilika Kimtindo, Asema Atafunguka Zaidi Kwenye Documentary

Msanii nyota kutoka Kenya, Victoria Kimani, amewasha moto mitandaoni baada ya kufichua muonekano mpya wa kipara, hatua aliyoiita mwanzo wa sura mpya katika maisha yake. Kupitia mtandao wa Instagram, alichapisha picha mbalimbali zenye ujumbe wa kina, akieleza safari ya kujitambua, kuamka kiroho, na kuenzi urithi wa Kiafrika. Katika mfululizo wa picha hizo, alionesha taswira ya simba akifuatisha na ujumbe wa kutambua nguvu ya kipekee ya mtu binafsi, mawingu yaliyochanwa na mwanga kama ishara ya kujifunua katika hali halisi, na picha za viongozi wa Kiafrika kama Mandela, Nyerere, Kenyatta na Kofi Annan, kuenzi uongozi na roho ya bara la Afrika. Aidha, alidokeza kuwa maudhui hayo yatakuwa sehemu ya filamu anayotarajia kuzungumzia hivi karibuni, huku akimalizia na picha iliyoandikwa “A course by Victoria Kimani”, kuashiria ujio wa mradi maalum kutoka kwake. Mashabiki wake wameonesha hamasa kubwa, wakisubiri kwa hamu kile kinachofuata kutoka kwa msanii huyo anayejulikana kwa ubunifu wa hali ya juu na maudhui yenye maana ya kina.

Read More