Vindee Aomba Radhi Baada ya Kudai Ana Ukaribu na IShowSpeed

Vindee Aomba Radhi Baada ya Kudai Ana Ukaribu na IShowSpeed

Prankster kutoka Kenya Vindee ameomba radhi Wakenya baada ya kudai awali kuwa alikuwa katika mawasiliano na staa wa mitandao ya kijamii, IShowSpeed, kuhusiana na ziara yake nchini humo. Kupitia taarifa rasmi aliyotoa mtandaoni, Vindee amesema lengo lake halikuwa kuwapotosha watu wala kutafuta kiki, akisisitiza kuwa ni mzaha uliotoka nje ya muktadha uliokusudiwa. Ameongeza kuwa licha ya watu mbalimbali kumshawishi na hata kujaribu kumuonga kwa maelfu ya pesa, alikataa kabisa kwa kuwa alihofia hatua hiyo ingemletea matatizo makubwa baadaye. Vindee amesema amejifunza kutokana na tukio hilo na kuahidi kuwa makini zaidi na maudhui anayotoa kwa umma, akitoa wito kwa mashabiki na umma kwa ujumla wasimchukulie vibaya. Kauli ya Vindee imekuja muda mfupi baada ya video yake kusambaa mitandaoni, ikimuonyesha akishindwa hata kumsalimia IShowSpeed walipokutana ana kwa ana, hali iliyozua maswali mengi kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakiamini kuwa wawili hao walikuwa wakizungumza mara kwa mara.

Read More
 Content Creator wa Kenya Apokea Kipigo Kikali, Apoteza Jino na Simu Kuvunjwa

Content Creator wa Kenya Apokea Kipigo Kikali, Apoteza Jino na Simu Kuvunjwa

Content creator mmoja wa Kenya anayefahamika kwa jina la Vindee, ameripotiwa kushushiwa kipigo kikali na wananchi baada ya kuwafanyia mzaha (prank) wakiwa katika shughuli zao za kila siku za kutafuta riziki. Kwa mujibu wa mashuhuda, content creator huyo alikuwa akirekodi maudhui ya mzaha bila ridhaa ya wahusika, jambo lililozua hasira miongoni mwa wananchi waliolengwa. Inadaiwa kuwa mzaha huo ulitafsiriwa kama dharau na kero, hali iliyopelekea mvutano uliogeuka kuwa vurugu na kusababisha majeraha makubwa pamoja na uharibifu wa vifaa vya kazi. Katika tukio hilo, content creator huyo alipigwa vibaya kiasi cha kupoteza meno, huku simu iliyokuwa ikitumika kurekodi maudhui hayo ikipasuliwa na kuharibiwa vibaya. Baada ya video na picha za tukio kusambaa mitandaoni, mjadala mpana umeibuka kuhusu maudhui ya prank na mipaka yake, huku wengi wakitoa wito kwa watengenezaji wa maudhui kuwa waangalifu zaidi na kuheshimu watu, hasa wanapokuwa kwenye shughuli zao za kujipatia kipato.

Read More