Content creator mmoja wa Kenya anayefahamika kwa jina la Vindee, ameripotiwa kushushiwa kipigo kikali na wananchi baada ya kuwafanyia mzaha (prank) wakiwa katika shughuli zao za kila siku za kutafuta riziki.
Kwa mujibu wa mashuhuda, content creator huyo alikuwa akirekodi maudhui ya mzaha bila ridhaa ya wahusika, jambo lililozua hasira miongoni mwa wananchi waliolengwa.
Inadaiwa kuwa mzaha huo ulitafsiriwa kama dharau na kero, hali iliyopelekea mvutano uliogeuka kuwa vurugu na kusababisha majeraha makubwa pamoja na uharibifu wa vifaa vya kazi.
Katika tukio hilo, content creator huyo alipigwa vibaya kiasi cha kupoteza meno, huku simu iliyokuwa ikitumika kurekodi maudhui hayo ikipasuliwa na kuharibiwa vibaya.
Baada ya video na picha za tukio kusambaa mitandaoni, mjadala mpana umeibuka kuhusu maudhui ya prank na mipaka yake, huku wengi wakitoa wito kwa watengenezaji wa maudhui kuwa waangalifu zaidi na kuheshimu watu, hasa wanapokuwa kwenye shughuli zao za kujipatia kipato.