Vinka akanusha tuhuma za kufanya upasuaji wa kuongeza makalio

Vinka akanusha tuhuma za kufanya upasuaji wa kuongeza makalio

Mwimbaji wa Swangz Avenue Vinka bila shaka ni moja kati ya wasanii wa kike wenye muonekano mzuri kwa sasa nchini Uganda. Hata hivyo, hali hiyo haikuwa hivyo miaka michache iliyopita kabla ya kupata ujauzito na kujifungua mtoto wake wa kiume. Naam, kutokana na mabadiliko yake ya mwili ambayo hayakutarajiwa ikiwemo kuongezeka kwa ukubwa wa makalio yake, mashabiki wamekuwa wakidai kwamba alifanyiwa upasuaji. Lakini wakati akimjibu shabiki kwenye majukwaa yake ya mitandao ya kijamii, Vinka amepuuzilia mbali madai hayo kwa kusema kuwa hana muda wa kuwaaminisha walimwengu kuwa viungo vya mwili wake ni asili. “Naweza kuthibitisha kuwa ni halisi lakini sina haja ya kufanya hivyo,” alimjibu shabiki mmoja aliyedai kuwa makalio yake yalikuwa bandia. Vinka amekuwa akipakia picha za kusisimua kwenye mitandao yake ya kijamii ambazo zinazidi kuwafanya wanaume wengi kutokwa na udenda na kushindwa kujizuia.

Read More
 Swangz Avenue yamfuta kazi meneja wa Vinka kwa madai ya utapeli

Swangz Avenue yamfuta kazi meneja wa Vinka kwa madai ya utapeli

Lebo ya Swangz Avenue imethibitisha kumfuta kazi meneja wa msanii wao Vinka kwa madai ya kufuja pesa za booking. Katika taarifa iliyotolewa na Swangz Avenue, meneja huyo aitwaye Navit Miles hafanyi kazi tena na Lebo hiyo huku ikionya umma kutoshirikiana na Navit kwenye biashara yeyote inayohusiana na Swangz Avenue. Chanzo cha karibu na lebo hiyo kimefichua kuwa jamaa huyo alitimuliwa kazi kwa ubadhirifu wa pesa za msanii wake Vinka ikizingatiwa kuwa yeye ndiye alikuwa anaratibu shows za msanii huyo. “Ni kuhusu fedha. Mabosi wake hawakufurahishwa na jinsi alivyoshughulikia malipo aliyopewa na mteja kwa ajili ya kupata huduma za Vinka. Hakuwasilisha pesa zote kwa kampuni hiyo,” chanzo kilifichua. Swangz Avenue ni lebo kubwa zaidi nchini Uganda na kwa sasa ina wasanii wanne waliosainiwa katika lebo hiyo, Winnie Nwagi, Vinka, Azawi na Zafarani.Wasanii hao kila mmoja ana timu ambayo inajumuisha meneja na wasaidizi.

Read More
 Mwanamuziki kutoka Uganda Vinka atangaza ujio mpya 2023

Mwanamuziki kutoka Uganda Vinka atangaza ujio mpya 2023

Msanii kutoka nchini Uganda Vinka ametangaza ujio wa album mpya mwaka wa 2023 ikiwa ni miaka tatu zimepita tangu awabariki mashabiki zake na album iitwayo Love Doctor iliyotoka mwaka 2019 Vinka ambaye amekuwa kwenye muziki kwa takriban miaka sita amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kupokea album yake mpya ambayo kwa sasa anaifanyia kazi. Aidha Hitmaker huyo wa Thank God amesema kwa sasa hana mpango wa kuja na tamasha lake la muziki kama namna wasanii wengine nchini uganda wanavyofanya ikizingatiwa kuwa ana majukumu ambayo anayashughulikia kwenye muziki wake. Lebo ya Swangz Avenue kwa mwaka huu pekee imefanya matamashs mawili makubwa kwa wasanii wake Azawi na Winnie Nwagi ambao walijunga na lebo hiyo mwaka wa 2019 baada ya Vinka. Hata hivyo tetesi za ndani kutoka kwa watu wa karibu na vinka zinadai kuwa huenda mrembo huyo akaanda tamasha lake la muziki mwaka ujao.

Read More
 VINKA AKANUSHA KUWA KWENYE BIFU NA AZAWI

VINKA AKANUSHA KUWA KWENYE BIFU NA AZAWI

Msanii wa Swangz Avenue Vinka amekanusha madai ya kuwa kwenye ugomvi na msanii mwenzake Azawi. Katika mahojiano yake hivi karibuni vinka amesema madai hayo hayana msingi wowote kwa kuwa yanachochewa na baadhi ya watu wasiokuwa shughuli ya kufanya maishani. Hitmaker huyo wa ngoma ya “One Bite” amesema kuwa kama kweli angekuwa na ugomvi na azawi angemuunga mkono kwenye harakati zake za kutangaza onesho lake litakalofanyika hivi karibuni. Hata hivyo amesema yeye na Azawi ni marafiki wakubwa hivyo wameelekeza nguvu zao zote kwenye suala la kuupeleka muziki wa uganda kimataifa. Kauli ya Vinka imekuja mara baada ya uvumi kusambaa mtandaoni kuwa ana bifu na Azawi licha ya kwamba wote wamesainiwa kwenye lebo moja ya muziki.

Read More
 VINKA AKANUSHA KUFANYIWA SURGERY KUBADILISHA MWILI WAKE

VINKA AKANUSHA KUFANYIWA SURGERY KUBADILISHA MWILI WAKE

Mwanamuziki wa Swangz Avenue  Vinka amekanusha madai yanayosambaa mtandaoni kuwa alifanyiwa upasuaji kwa ajili ya kuongeza makalio yake. Katika moja ya onesho lake huko nchini Uganda Vinka amewaambia mashabiki zake kuwa amepata mabadiliko makubwa kwenye mwili wake mara baada ya kujifungua mtoto wake mwishoni mwa wa 2021 jambo analodai limempelekea kuanza mazoezi ya kuweka mwili wake sawa. Utakumbuka kipindi vinka anaanza muziki miaka kadhaa iliyopita alikuwa na mwili mdogo kiasi cha watu kuanza kumfananisha na mwanaume lakini katika siku za hivi karibuni amebadilika kimuonekano jambo ambalo limezua maswali mengi miongoni mwa mashabiki zake wengi wakihoji huenda amefanyiwa surgery kuongeza baadhi ya viungo vya mwili wake.

Read More
 VINKA ATIA SAINI MKATABA MPYA NA LEBO YA SWANGZ AVENUE

VINKA ATIA SAINI MKATABA MPYA NA LEBO YA SWANGZ AVENUE

Mwanamuziki kutoka Uganda Vinka ametia saini mktaba mpya na lebo ya muziki ya Swangz Avenue ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu msanii mwenzake Winnie Nwagi aongeze mkataba wake na lebo hiyo. Vinka ameweka wazi habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram akitia wino mkataba wake wa miaka 5 na lebo hiyo kwenye hafla iliyoshuhudiwa na Afisa mkuu mtendaji wa Swangz Avenue Julius Kyazze pamoja na wakili wake Joel Plus. Kulingana na Swangz Avenue Vinka bado ni msanii wa Sony music Africa ambaye ana mkataba mrefu nao ila swangz avenue itabaki kuwa uongozi wake kwa niaba ya Sony music. Lakini pia lebo hiyo imekanusha taarifa za kuwatema wasanii wake wakongwe baada ya kuwasaini wasanii wapya kama Zafarah na Azawi. Swangz avenue imekuwa ikisimamia muziki wa Vinka tangu mwaka wa 2016 na mwaka wa 2018 Vinka alisaini mkataba na sony music. Utakumbuka mpaka sasa Swangz Avenue ina jumla ya wasanii 4 ambao ni Winnie Nwagi, Azawi, Vinka na Zafaran ambaye alisainiwa majuzi na lebo hiyo.

Read More
 VINKA AKANUSHA MADAI YA KUFICHA UJA UZITO

VINKA AKANUSHA MADAI YA KUFICHA UJA UZITO

Mwanamuziki wa Swangz Avenue Vinka amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa alificha uja uzito wake kwa umma mwaka wa 2021. Katika mahojiano yake hivi karibuni, Vinka amesisitiza kwamba alifanya performances kwenye sherehe za harusi hadi pale alipokaribia kujifungua huku akisema kwamba alikuwa pia akichapisha picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa mjamzito. Hitmaker huyo wa Thank God amesema baada ya kujifungua ilimchukua mwezi mmoja kurudi kuendeleza harakati zake za kuwapa mashabiki zake burudani kwani kuna watu wengi walimpa mialiko ya kutumbuiza kwenye sherehe zao za harusi. Vinka alibarikiwa na mtoto wake wa kike mwaka 2021 jambo lilowaacha mashabiki zake na mshangao kwani walikuja wakajua alikuwa mja mzito  baada ya kujifungua.

Read More
 VINKA AKANUSHA ISHU YA KUWAKODISHA NA WALINZI

VINKA AKANUSHA ISHU YA KUWAKODISHA NA WALINZI

Female singer kutoka Uganda Vinka amekanusha madai ya kuwakodisha walinzi kwa ajili ya kumpa usalama wakati wa shows zake. Kupitia ukurasa wake wa twitter vinka amesema kuwa wanaume wawili ambao huandamana nao kwenye shows zake sio walinzi wake bali ni timu inayounda menejiment yake. Hitmaker huyo wa “Thank God” amewataka wanablogu nchini Uganda kukoma kueneza taarifa za uongo kuwa amekodisha mabouncers kwa ajili ya kumpa walinzi. Kauli ya Vinka imekuja mara baada ya kurasa moja ya udaku kuikejeli picha yake kwenye mtandao wa twitter kwa kusema kwamba mmoja wa walinzi wa vinka anahitaji usalama kutokana na kuwa na mwili mdogo.

Read More
 MSANII WA SWANGZ AVENUE VINKA ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LAKE LA MUZIKI NCHINI UGANDA

MSANII WA SWANGZ AVENUE VINKA ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LAKE LA MUZIKI NCHINI UGANDA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Vinka, ametangaza  mpango wa kuja na tamasha la muziki ndani ya mwaka huu wa 2022. Vinka ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Fimbo amethibitisha hilo kwenye moja ya performance yake huko Munyonyo nchini Uganda wikiendi iliyopita ambapo amesema onesho hilo ni kwa ajili ya kusherekea  miaka 5 ya uwepo wake kwenye muziki pamoja na mashabiki zake. Hata hivyo msanii huyo wa Swangz Avenue hajaweka wazi ni lini hasa atakuja na onesha lake la muziki ila ni jambo la kusubiriwa. Utakumbuka Vinka alianza safari ya muziki chini lebo ya muziki ya Swangz Avenue mwaka wa 2017 alipoachia singo yake  ya kwanza iitwayo  Levels ikafuatwa na Stylo aliyomshirikisha bosi wake wa zamani Irene Ntale. Tangu kipindi hicho amekuwa na muendelezo wa kuachia nyimbo kali bila kupoa jambo ambalo limempelekea kushinda tuzo nyingi nchini Uganda lakini pia imempelekea kuingia ubia wa kufanya kazi na kampuni ya Sony Music, tawi la Afrika.

Read More