VIVIAN AWAPA SOMO WASANII WA KIKE NCHINI KENYA

VIVIAN AWAPA SOMO WASANII WA KIKE NCHINI KENYA

Msanii nyota nchini Vivian amewapa somo mastaa wa kike kwa kuwataka wajitume ili kujiletea maendeleo kwa kuwa muda wa kutumiwa kingono na wanaume umepita. Akizungumza na Mungai Eve, Vivian amesema kuwa baadhi ya wasanii wamekuwa wakijiweka nyuma na wakati mwingine kukubali kutumiwa kingono ili watoke wakati uwezo wanao. Vivian ambaye anafanya vizuri na wimbo wake uitwao Chachisha aliomshirikisha Sosuun amesema dhana ya mwanamke shujaa kwake ni yule anayepambana kufanikisha kila kitu huku akisisitiza kwamba mwanamke anaweza kuwa kiongozi, mwalimu au kufanya kazi yoyote iwapo akidhamiria kupambana. Hata hivyo amewataka wanawake kuondoa dhana ya kuwezeshwa na badala yake wapambane kutunza uanamke wao.

Read More
 SOSUUN AMVUA NGUO VIVIAN KWA MADAI YA KUMVUNJIA HESHIMA

SOSUUN AMVUA NGUO VIVIAN KWA MADAI YA KUMVUNJIA HESHIMA

Rapa wa kike nchini Sosuun amemsuta vikali msanii vivian kwa madai ya kuvumnjia heshima aliposema kwenye moja ya post yake kwenye mtandao wa Instagram kuwa familia ya msanii huyo ndio imeua kipaji chake cha muziki. Kwenye post hiyo vivian alitoa rai kwa sosuun arudi tena kwenye muziki kutokana na mashabiki kukosa nyimbo zake kwa muda ambapo alienda mbali zaidi kudai kuwa hatua ya sosuun kupotea kwenye muziki imetokana na yeye kujikita zaidi kwenye masuala ya familia, jambo ambalo amedai limemponza kimuziki. Sasa Kupitia instagram wake Sosuun aliibuka na kutupia maneno mazito vivian kwa kusema kwmbaa aache  kumfuatilia maisha yake na badala yake amzalie mume wake watoto aone kama atabaki kwenye muziki wake ambapo amejitapa kwa kusema kwamba amemzidi kimuziki licha ya ukimya wa miaka 10 kwenye muziki wake. Haikushia hapo Sosuun alienda mbali zadi na kumtaka vivian abadili muonekano wake wa kisanii huku akisema kwamba msanii huyo anajishusha kimuziki kwa  kuvalia mavazi yasioendana na brand yake licha ya kuwa mwiimbaji mzuri. Hata hivyo hatua ya wawili hao kutupiana maneno makali mitandaoni imeonekana kuibua maswali miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ambapo baadhi ya wamemnyoshea kidole cha lawama vivian kwa kumvunjia heshima sosuun kwa kuyaweka mapungufu yake mtandaoni huku wengine wakihoji kuwa huenda wawili hao wanatengeneza mazingira ya kuzungumziwa ili waweze kuachia ngoma ya pamoja.

Read More
 MSANII WA KIKE KUTOKA KENYA VIVIAN AKIRI KUPITIA MAGUMU KIMAISHA

MSANII WA KIKE KUTOKA KENYA VIVIAN AKIRI KUPITIA MAGUMU KIMAISHA

Msanii wa kike nchini Vivian anaendelea kufunguka kuhusu maisha yake ya ndani, amedai kwamba katika kipindi cha miezi 6 iliyopita amekuwa kwenye hali ngumu kimaisha. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Vivian amesema wiki hii iliyopita ndio mambo yalianza kumuendea murama huku akidai kuwa amepoteza imani kabisa kwenye upendo wa kweli kwani alivunjwa moyo na kuumizwa vibaya jambo ambalo amedai limemuacha hoi. Haikushia hapo mrembo huyo alienda mbali zaidi na kusema kwamba amekuwa akitia bidii kuhakikisha kwamba kila kitu kinaenda sawa huku akisisitiza kuwa ana imani mambo yatakuwa mazuri hivi karibuni kwani anaamini dunia itampa nafasi tena ya kujipenda mwenyewe. Hata hivyo Vivian hajaweka wazi kinachosumbua maishani ila ujumbe wake umeibua maswali mengi miongoni mwa watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii ambapo wengi wamehoji kuwa huenda ndoa ya Vivian na mume wake Sam West imeingiwa na ukungu.

Read More