VIVIAN TENDO AKANUSHA ISHU YA KUTOKA KIMAPENZI NA MUSA ATAGENDA

VIVIAN TENDO AKANUSHA ISHU YA KUTOKA KIMAPENZI NA MUSA ATAGENDA

Msanii wa kike nchini Uganda Vivian Tendo amekanusha tuhuma za kuwa kwenye mpango wa kufunga ndoa ya siri na bosi wa Wakiso Giants Musa Atagenda. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Tendo amesema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Musa Atagenda kama inavyodaiwa mitandaoni ambapo ameenda mbali zaidi na kupuzilia mbali mipango ya kuhalalisha mahusiano yao ya kimapenzi. Hitmaker huyo wa  ngoma ya “Timango” amesema hana mpango wa kuingia kwenye ndoa hivi karibuni kwani kwa sasa ameelekeza nguvu zake kwenye suala la kuupeleka muziki kimataifa. Kauli ya Vivian Tendo imekuja mara baada ya walimwengu kuhoji kuwa huenda mrembo huyo anatoka kimapenzi na mfanyibiashara huyo kufuatia kuonekana pamoja kwenye moja ya video iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikiwaonyesha wakiwatakia mashabiki zao mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Read More
 YESE OMAN RAFIKI AKIRI KUUMIZWA N KITENDO CHA MSANII VIVIAN TENDO KUJIONDOA ROUTE ENTERTAINMENT

YESE OMAN RAFIKI AKIRI KUUMIZWA N KITENDO CHA MSANII VIVIAN TENDO KUJIONDOA ROUTE ENTERTAINMENT

Msanii na mwaandishi wa nyimbo kutoka nchini Uganda Oman Rafiki amefunguka na kudai kuwa aliumizwa na kitendo cha msanii Vivian Tendo kujiondoa kwenye lebo ya muziki ya Route Entertainment. Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni Oman Rafiki amesema licha ya kuumizwa na kitendo cha mrembo huyo kumkimbia hatokataa tamaa ya kuwasajili wasanii wapya wenye vipaji kwenye lebo hiyo. Oman Rafiki ambaye pia ni Meneja wa wasanii amesema amejifunza umuhimu wa kuwa na mkataba wa maelewano na msanii yeyote atakajiunga na lebo ya route Entertainment kwani itamsaidia sana wakati msanii husika atajiondoa ghafla kwenye lebo hiyo. Inadaiwa kuwa Oman rafiki na vivian tendo wamefanya kazi kwa pamoja tangu mwaka wa 2018 kwa makubaliano ya urafiki wa kimapenzi. Hata hivyo inasemekana Vivian Tendo na Oman Rafiki wana mpango wa kuelekea mahakamani kuhusiana na hakimiliki ya muziki na masuala mengine.

Read More
 MWANAMUZIKI WA UGANDA VIVIAN TENDO ADAI MAISHA YAKE YAMO HATARINI

MWANAMUZIKI WA UGANDA VIVIAN TENDO ADAI MAISHA YAKE YAMO HATARINI

Mwanamuziki wa kike kutoka nchini uganda Vivian Tendo amefunguka na kudai kuwa maisha yake yamo hatarini. Kupitia ukurasa wake wa Instagram mrembo huyo ameshare audio clip ya meneja wake wa zamani Oman rafiki akimtolea vitisho na kuweka wazi kuwa anaishi kwa hofu kwani huenda meneja wake huyo akamuangamiza. Hitmaker huyo wa “Timango” amesema amejaribu kunyamazia suala hilo kwa muda na hata kukwepa interviews mbali mbali ili asizungumzie vibaya uongozi wake wa zamani lakini maji yamezidi unga kwa upande wake ambapo amewataka mashabiki na wanafamilia wake kumuwajibisha Oman Rafiki ikitokea amefariki ghafla. Kauli ya mrembo huyo inakuja siku chache baada ya Oman Rafiki kunukuliwa kwenye moja ya interviews akisema kuwa ana mpango wa kumfungulia mashtaka viviam tendo kwa madai ya kukiuka mkataba wake na lebo ya Route Entertainment. Utakumbuka Vivian Tendo aliachana na uongozi wake wa Route Entertainment mwezi disemba mwaka wa 2021 kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi lakini inaonekana meneja wake wa zamani Oman Rafiki hataki kumuacha mrembo huyo salama kwani amewekeza pesa zake nyingi kwenye muziki wake.

Read More