Wahu: Nilihisi Uchungu Kusikia Watoto Wakisema Siwezi Kuzaa Tena

Wahu: Nilihisi Uchungu Kusikia Watoto Wakisema Siwezi Kuzaa Tena

Mwanamuziki wa Kenya Wahu Kagwi ameeleza kwa hisia namna watoto wake walivyokuwa wakiomba kwa muda mrefu wapate mdogo wao, lakini baadaye wakakata tamaa wakiamini mama yao ni mkubwa sana kuweza kuzaa tena. Kwenye mahojiano na Willow Health Media, Wahu amesema maombi ya watoto wake yalikuwa ya dhati, wakitamani sana kupata mtoto wa mwisho katika familia yao. Kwa muda mrefu, alikuwa akiwaasikia wakiwa chumbani mwao wakiomba kwa Mungu awape mdogo wao. Alikumbuka tukio la miaka iliyopita ambapo binti yake mkubwa alimweleza mdogo wake kuwa haamini kama hilo lingetokea kwa sababu alihisi mama yao ni mkubwa sana kuweza kupata mtoto mwingine. Kauli hiyo iliwafanya waache kabisa kuzungumzia jambo hilo, na wakaonekana kukata tamaa. Hata hivyo, licha ya watoto wake kupoteza matumaini, familia hiyo baadaye ilibarikiwa kwa mtoto wa tatu, jambo lililowaletea furaha kubwa na kutimiza ndoto ya watoto hao kwa njia ya kushangaza. Wahu na mumewe Nameless wameendelea kuwa mfano wa kuigwa katika malezi, wakionesha mapenzi ya kweli kwa watoto wao na maisha ya kifamilia yaliyojaa mawasiliano na mshikamano. Kisa hiki kimetafsiriwa na wengi kuwa ujumbe wa tumaini na imani kwa ndoto za watoto ambazo huenda zikawa kimya, lakini bado huwa na uzito mkubwa.

Read More
 Nameless awajibu kisomo wanaomshinikiza kupata mtoto wa kiume

Nameless awajibu kisomo wanaomshinikiza kupata mtoto wa kiume

Msanii nyota nchini Nameless amewajibu walimwengu wanaomshinikiza kuzaa mtoto wa kiume kama njia ya kudhihirisha uanaume wake katika jamii. Akimjibu shabiki mmoja aliyemtaka aweke mkakati wa kumpata mtoto wa kiume na mke wake Wahu kwenye mtandao wa Facebook, Nameless amesema anajivunia kuwa baba ya watoto wa kike na lengo lake kwa sasa ni kuwalea mabinti zake kwenye mazingira yatakayowapa fursa ya kuishi na watu vizuri. Hitmaker huyo wa “Teamo” amewataka mashabiki kuacha kasumba ya kufuata mila zilizopitwa na wakati na badala yake wakumbatie utandawazi kama njia mojawapo ya kuendana na nyakati zilizopo. “Tafuta kijana boss…..Your legacy…..We Africans”, Shabiki aliandika kwenye mtandao wa Facebook ambapo Nameless alishuka kwenye uwanja wa comment na kuandika “”Saa zingine tunajiangusha na traditions that are outdated. Let’s evolve buana” Ikumbukwe Nameless na Wahu ambao wamekuwa kwenye ndoa tangu mwaka 2005, kwa pamoja wamebarikiwa kuwapata mabinti watatu ambao ni Tumiso, Nyakio na Shiru ambaye alizaliwa juzi kati.

Read More
 Wahu na Nameless wapata mtoto wa kike

Wahu na Nameless wapata mtoto wa kike

Lejendari wa muziki nchini  Nameless  amethibitisha kuwa mke wake Wahu amejifungua mtoto wa kike. Nameless ameeleza furaha yake kupitia mitandao yake ya kijamii kwa Wahu kujifungua salama, akimshukuru Mungu pamoja na mashabiki zake ambao wamekuwa mstari wa mbele kuwaombea dua kwa kusema kuwa mke yupo tayari kwa majukumu ya kumlea mtoto wao Aidha amesema mtoto huyo wa kike ambaye amepewa jina la kumuenzi dada yake mkubwa kulingana na tamaduni za jamii ya Kikuyu, anaitwa Shiru. Ni hatua ambayo imepokelewa kwa furaha na mastaa wenzake kutoka Kenya ambao walitupia comment zao kwenye posti yake wakimtakia heri pamoja na mke wake Wahu. Huyu anakuwa mtoto wa tatu kwa Nameless na Wahu Kagwi ambao wametimiza miaka 17 wakiwa mume na mke ikizingatiwa tayari katika ndoa yao wamebahatika kupata watoto wawili, wote wakiwa wakike.

Read More
 Wahu na Nameless waweka wazi jinsia ya mtoto wao

Wahu na Nameless waweka wazi jinsia ya mtoto wao

Staa wa muziki nchini Wahu ameweka wazi jinsia ya mtoto wake wa tatu ambaye atazaliwa hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amechapisha video ya hafla ya utambulisho wa jinsia ya mtoto wao na kusindikiza na maneno yanayosomeka “BabaGalz Chairman honored, excited and ready for Duty! Ujumbe huo umetafsiri moja kwa moja na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa Wahu na mume wake Nameless wanatarajia kumpata mtoto wa kike. Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali wamewapongeza wawili hao kwa hatua hiyo wakati huu wapo mbioni kumkaribisha mwanafamilia mwingine. Utakumbuka juzi kati taarifa zilisambaa mtandaoni zikidai kuwa huenda Wahu alijifungua kwa siri kutokana na jumbe alizokuwa anachapisha kwenye mtandao wake wa Instagram.

Read More
 WAHU NA NAMELESS WASHEREKEA MIAKA 17 YA NDOA

WAHU NA NAMELESS WASHEREKEA MIAKA 17 YA NDOA

Wanamuziki David Mathenge maarufu kama Nameless na Wahu Kagwi wametimiza miaka 17 ya ndoa na miaka 25 tangu wayaanze mahusiano yao. Wawili hao ambao walianza mahusiano yao mwaka 1997 walifanikiwa kufunga ndoa mwaka 2005 na katika ndoa yao wamebahatika kupata watoto wawili, wote wakiwa wakike. Leo, Septemba 10 ni anniversary yao, ambapo wametimiza miaka 12 wakiwa mke na mume. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nameless ambaye ndiye mume wa Wahu ameandika haya.. “Happy Anniversary Babe! 17 years today since we said ” I DO!” and 25 years since our first date! And you still the ONE ! Just alittle heavier !! Thank you for taking this journey of life with me! ” Ndoa ya wanamuziki hao imedumu muda mrefu kinyume na matarajio ya wengi kutokana na jinsi watu maarufu wamekuwa wakiacha ndoa zao ulimwenguni kote. Utakumbuka kwa sasa Nameless na Wahu wanatarajia kupata mtoto wao wa tatu hivi karibuni.

Read More
 NAMELESS NA WAHU WANATARAJIA MTOTO WA TATU

NAMELESS NA WAHU WANATARAJIA MTOTO WA TATU

Wanamuziki David Mathenge maarufu kama Nameless na Wahu Kagwi wametangaza kwamba wanatarajia mtoto wao wa tatu. Wawili hao walitoa tangazo hilo kupitia video ambayo waliichapisha kwenye mitandao ya kijamii. Tumiso ndiye kifungua mimba wa wanamuziki hao ambao walifunga ndoa mwaka 2005 na wa pili ni Nyakio. Ndoa ya wanamuziki hao imedumu muda mrefu kinyume na matarajio ya wengi kutokana na jinsi watu maarufu wamekuwa wakiacha ndoa zao ulimwenguni kote. Utakumbuka kwa sasa Wahu na Nameless wanafanya vizuri na wimbo wao mpya uitwao Deep, wimbo ambao ni wa sita kutoka kwenye album yao ijayo iitwayo MZ. Tayari wameachia nyimbo kama This Love Ya Wahu, This Love Ya Nameless, Te Amo, Feeling na Back it Up.

Read More
 WAHU AKOSHWA NA SHABIKI YAKE MLEMAVU,ACHANGISHA SHILLINGI 180,000 KUMSAIDIA

WAHU AKOSHWA NA SHABIKI YAKE MLEMAVU,ACHANGISHA SHILLINGI 180,000 KUMSAIDIA

Msanii wa muziki nchini Wahu Kagwi amefanikiwa kuchangisha takriban shillingi elfu 180 kwa ajili ya shabiki yake mmoja anayefahamika kama Eunice. Eunice ambaye ana changamoto ya ulemavu alikuwa anahitaji kiti cha magurudumu ambacho kinatumia umeme kufanikisha matembezi yake. Wahu alivutiwa na Shabiki huyo aliposhiriki shindano la tiktok la wimbo wake wa back it up, wimbo ambao uliuachia mwezi oktoba mwaka huu akiwa amemshirikisha Nameless. Baada ya kuuguswa na ukarimu wa mashabiki zake Wahu kupitia ukurasa wake wa Instagram alitangaza kusitisha mchango huo baada ya kufikisha shillingi elfu 180 ambapo ametumia fursa hiyo kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao walimuonyesha Eunice ambaye anaishi na changamoto ya ulemavu. Ikumbukwe Eunice pamoja washirika na wenzake kwenye challange ya wimbo Back It Up katika mtandao wa Tiktok walialikwa kwenye tamasha la Oktoba Fest la Wahu na Nameless na ndipo Wahu alipata wasaa mzuri wa kunzungumza na Eunice ambapo alifunguka mengi yanayomsibu.

Read More