Video ya “Kumbaba” Yaondolewa YouTube kwa Sababu za Hakimiliki

Video ya “Kumbaba” Yaondolewa YouTube kwa Sababu za Hakimiliki

Video ya wimbo maarufu “Kumbaba” wa kundi la rap kutoka Kenya, Wakadinali, imeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kufuatia madai ya ukiukwaji wa hakimiliki. Hatua hiyo imezua mazungumzo makubwa miongoni mwa mashabiki wa kundi hilo, ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuonyesha mshangao na kutoridhishwa na tukio hilo. Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa, video hiyo ambayo ilipata umaarufu mkubwa kutokana na mashairi yake ya kipekee na ubunifu wa Wakadinali, ilishutumiwa kwa kutumia vipengele vinavyodaiwa kuwa na hakimiliki bila idhini. Hata hivyo, haijabainika wazi ni ni nani au taasisi ipi iliyowasilisha malalamiko hayo kwa YouTube. Mashabiki wameeleza masikitiko yao, wengi wakisisitiza kuwa “Kumbaba” ilikuwa kati ya kazi bora zaidi za Wakadinali na mchango mkubwa katika kuendeleza hip hop ya mitaani nchini. Baadhi wamehoji kwa nini masuala ya hakimiliki hayakutatuliwa kabla ya video hiyo kuondolewa, wakihofia huenda hatua hiyo ikapunguza kasi ya ukuaji wa kazi za wasanii wa hapa nyumbani. Wakadinali, ambao wanajulikana kwa midundo yao mizito na mashairi yanayochora picha halisi ya maisha ya mitaani, bado hawajatoa kauli rasmi kuhusu sakata hilo. Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu kuona iwapo video ya “Kumbaba” itarejeshwa mtandaoni au iwapo kundi hilo litachukua hatua nyingine ya kisheria au kiubunifu ili kulinda kazi zao.

Read More
 Wakadinali Waachia Albamu Mpya “Victim of Madness 2.0” Yenye Ngoma 22

Wakadinali Waachia Albamu Mpya “Victim of Madness 2.0” Yenye Ngoma 22

Kikundi maarufu cha muziki wa hip-hop kutoka Kenya, Wakadinali, kimetoa rasmi albamu yao mpya inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki, “Victim of Madness 2.0”. Albamu hii ina jumla ya nyimbo 22, zenye mchanganyiko wa mitindo na maudhui ya kina yanayoakisi maisha ya mtaa, changamoto za vijana, na hali halisi ya jamii. Katika albamu hiyo, Wakadinali wamewaleta pamoja baadhi ya majina makubwa na maarufu kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki, akiwemo gwiji wa hip-hop Kitu Sewer, rapa mkongwe Abass Kubaff, Masterpiece, Skilo, mwimbaji wa muziki wa kitamaduni Suzzana Owiyo, pamoja na wasanii wengine kama Pepela, Katapila, Sodough Doss, na Wakuu. “Victim of Madness 2.0” si tu mwendelezo wa kazi yao ya awali, bali pia ni uthibitisho wa ukuaji wao kisanaa na ujasiri wa kubuni muziki wenye maudhui halisi. Kwa mchanganyiko wa sauti kali, mashairi ya busara na uhalisia wa maisha ya kila siku, albamu hii imepokelewa kwa shangwe na mijadala mitandaoni tangu ilipozinduliwa. Mashabiki na wachambuzi wa muziki wameisifu kazi hiyo kwa ubunifu wake, ushirikiano wa kipekee, na uendelezaji wa utamaduni wa hip-hop barani Afrika. Wakadinali wameendelea kujijengea nafasi ya kipekee kama sauti ya mtaa inayovunja mipaka ya kawaida ya muziki. Albamu hii sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya muziki mtandaoni ikiwemo Spotify, Apple Music, Boomplay na YouTube, ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wao waliokuwa wakiisubiri kwa muda mrefu.

Read More
 Wakadinali waachia rasmi album yao mpya “NDANI YA COCKPIT 3”

Wakadinali waachia rasmi album yao mpya “NDANI YA COCKPIT 3”

Kundi la muziki wa hiphop nchini Wakadinali limeachia rasmi album yao mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wao. Album hiyo iitwayo NDANI YA COCKPIT 3 ina jumla ya ngoma 15 za moto huku wakiwa wamewashirikisha wasanii kama Khaligraph Jones, Wangechi, Kitu Sewer, Kalahari, McGijo na wengine kibao. NDANI YA COCKPIT 3 ni muendelezo wa Album yao ya mwaka 2017-18 “Ndani ya Cockpit 1 & 2” iliyokuwa na jumla ya singles 9 na 13 mtawalia. Hii ni Album yao ya nne baada ya “Victims of Madness” ya mwaka wa 2020 na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya kukisikiliza na kupakua muziki duniani ikiwemo Boomplay,Spotify na Apple Music. Wakadinali ni kundi la Hiphop kutoka nchini Kenya linaloundwa na wasanii watatu ambao ni Scar, Domani Munga, pamoja na Sewersydaa.

Read More
 ALBUM YA WAKADINALI “VICTIMS OF MADNESS” YAFIKISHA ZAIDI YA STREAMS MILLIONI 5 BOOMPLAY

ALBUM YA WAKADINALI “VICTIMS OF MADNESS” YAFIKISHA ZAIDI YA STREAMS MILLIONI 5 BOOMPLAY

Kundi la muziki wa Hiphop nchini Wakadinali anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na Albamu yao ya ” Victims of Madness ” ambayo tayari ina takriban mwaka mmoja tangu itoke rasmi. Good news ni kwamba Album ya ” victims of madness ”  imefanikiwa kufikisha  zaidi ya Streams millioni 5  kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay. Wakadinali ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwashukuru mashabiki zao kwa upendo ambao wanazidi kuwaonyesha kupitia kazi zao za muziki huku likiahidi kuendelea kuwapa burudani zaidi kwa kuachia sehemu ya 2 ya album hiyo. Ikumbukwe Album ya Victims of madness kutoka kwa kundi la Wakadinali iliachia rasmi machi 4 mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 15 ya moto.

Read More