“Siku Moja Tutazungumza Kuhusu ‘Diddy’ wa Kenya” – Rapper Wangechi Afichua Mada Nzito Kuhusu Tasnia ya Muziki

“Siku Moja Tutazungumza Kuhusu ‘Diddy’ wa Kenya” – Rapper Wangechi Afichua Mada Nzito Kuhusu Tasnia ya Muziki

Msanii wa muziki wa rap nchini Kenya, Wangechi, ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kuandika ujumbe wa kutatanisha unaoashiria kuwepo kwa unyonyaji na hujuma dhidi ya wasanii wa kike katika tasnia ya muziki humu nchini. Kupitia akaunti yake ya mtandao wa X, Wangechi alidokeza kuwa kuna mtu mashuhuri kwenye sekta ya muziki humu nchini anayefanana na mtayarishaji wa muziki wa Marekani, Diddy ambaye kwa miaka amezuia wasanii wa kike kutoka na kazi zao kutoka studio. “One day we shall speak about the Diddy of Kenya and how no female artist ever left that studio with their music.” (“Siku moja tutazungumza kuhusu Diddy wa Kenya na jinsi hakuna msanii wa kike aliyewahi kutoka katika studio hiyo na muziki wake.”) – aliandika Wangechi. Ingawa hakumtaja mtu yeyote kwa jina, kauli hiyo imeibua mijadala mikubwa kuhusu usalama, haki na usawa katika sekta ya muziki hasa kwa wasanii wa kike ambao kwa muda mrefu wamelalamikia ukosefu wa usaidizi wa haki na kuwepo kwa mazingira yenye unyanyasaji wa kiakili, kijinsia na kitaaluma. Mashabiki na wadau wa muziki wameanza kujiuliza ni nani “Diddy wa Kenya” anayetajwa, huku wengi wakihusisha ujumbe huo na visa vya awali vilivyoripotiwa na baadhi ya wanamuziki wachanga. Hadi kufikia wakati wa kuchapishwa kwa habari hii, Wangechi bado hajatoa maelezo zaidi, lakini ujumbe wake umeacha gumzo zito ambalo huenda likabadilisha mwelekeo wa mazungumzo kuhusu usalama, uhuru na haki za wasanii wa kike nchini Kenya.

Read More
 RAPA WANGECHI ADOKEZA UJIO WA ALBUM MPYA YA SCAR MKADINALI

RAPA WANGECHI ADOKEZA UJIO WA ALBUM MPYA YA SCAR MKADINALI

Rapa wa kike nchini Wangechi amedokeza kuwa member wa  kundi la Wakadinali, Scar Mkadinali ana mpango wa kuachia album yake mpya mwisho mwa mwezi huu wa Januari. Wangechi amethibitisha hilo kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram kwa kusema kwamba  album ya rapa huyo iitwayo Easy itaingia sokoni januari  24 mwaka huu. Hata hivyo hajaweka wazi idadi ya ngoma ambazo zitapatikana kwenye album hiyo ila Wangechi atakuwa moja kati ya wasanii ambao watashirikishwa kwenye album ya Scar Mkadinali. Ikumbukwe mwaka wa 2019 Wangechi na Scar Mkadinali waliachia singo yao ya pamoja inayokwenda kwa jina la Sana Sana.

Read More