WASANII WA P-UNIT WATIA NIA YA KUGOMBEA UONGOZI MWAKA 2022
Wasanii wanaounda kundi la P-Unit, Frasha na Gabu wametia nia ya kugombea nyadhifa za uongozi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022. Wawili hao wametangaza kuwa watawania viti vya uwakilisha wadi. Francis Aamisi maarufu kama Frasha amesema atasimama kiti cha uwakilisha wadi huko Athi River huku Gabriel Kagundu maarufu kama Gabu akiwania kiti cha uwakilishi wadi eneo la Kenyatta Golf Course mwaka wa 2022. Wasanii hao wanajiunga na wasanii wengine kama Prezzo na Reuben kigame ambao wametia nia ya kuwania uongozi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Read More