PRODYUZA WASHINGTON AKANUSHA KUYUMBA KIUCHUMI

PRODYUZA WASHINGTON AKANUSHA KUYUMBA KIUCHUMI

Prodyuza mkongwe Washington juzi kati alizua mjadala mtandaoni alipoandika ujumbe wa kuwashinikiza baadhi ya wasanii nchini Uganda kumlipa mirahaba ya nyimbo alizofanya nao kipindi cha nyuma. Ujumbe huo ulitafsiriwa na wengi kuwa huenda prodyuza huyo anapitia wakati mgumu kimaisha kutokana na kuyumba kiuchumi. Sasa kwenye mahojiano yake hivi karibuni Washington ameibuka na kukanusha madai ya kufulia kiuchumi kwa kusema kwamba alikuwa anajaribu kuwakingia kifua maprodyuza wachanga ambao wananyanyaswa kwenye muziki wapate haki yao. Kuhusu ishu ya wasanii kutomlipa pesa, Washington amesema waligharamia malipo ya huduma za studio ambayo ni tofauti kabisa na mirahaba ya nyimbo zao.

Read More
 PRODYUZA WA MUZIKI WASHINGTON AVULIA KIUCHUMI

PRODYUZA WA MUZIKI WASHINGTON AVULIA KIUCHUMI

Prodyuza wa muziki Washington ameripotiwa kuvunjika vipande vipande kwa kuwa hana chochote zaidi ya hali mbaya ya kiuchumi. Kupitia mitandao yake ya kijamii Washington ametoa ilani kwa wasanii wote aliofanya nao kazi kipindi cha nyuma kumlipa mirabaha ya kazi zake kutokana na kuyumba kiuchumi. Hata hivyo mkali huyo kutoka Uganda ametoa makataa ya saa 24 kwa wasanii hao kumlipa haki yake la sivyo atafuta nyimbo zao kwenye majukwaa ya kuuza na kusikiliza muziki mtandaoni. Kwa mujibu wa mitandao ya habari za burudani nchiniUganda, Washington anatajwa kuwa anapitia wakati mgumu kwa sasa kutokana na kutopata bookings kutoka kwa wasanii katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Read More