Mzozo Mpya Wazuka Kati ya Weasel na Mkewe Sandra Teta

Mzozo Mpya Wazuka Kati ya Weasel na Mkewe Sandra Teta

Mwanamuziki wa Uganda, Weasel Manizo, na mkewe Sandra Teta wamejikuta tena katika mzozo mkali, miezi miwili tu baada ya tukio la awali ambapo inadaiwa Teta alimgonga kwa gari. Tukio jipya limeibuka kupitia video iliyosambaa usiku wa kuamkia jana, ikimuonyesha Weasel akiwa katika hali ya taharuki huku akilia akiomba msaada. Katika video hiyo, Teta anaonekana akijaribu kumshambulia Weasel kwa kifaa kikali, wakati ndugu wa familia wakijitahidi kumzuia. Ingawa Teta alisikika akikanusha kumdhuru mumewe, bado haijabainika chanzo cha mzozo huo mpya. Weasel, akionekana mwenye hofu kubwa, alimshutumu mkewe kwa kumtesa na kumtaka aondoke nyumbani kwake, akisema hana tena amani naye. Hali hii imewafanya mashabiki na wadau wa muziki kuhoji mustakabali wa ndoa yao, hasa ikizingatiwa kuwa si mara ya kwanza wawili hawa kuingia katika ugomvi wa hadharani. Mnamo Julai mwaka huu, Teta alidaiwa kumgonga Weasel kwa gari katika baa moja eneo la Munyonyo, tukio lililosababisha msanii huyo kulazwa katika Hospitali ya Nsambya akiwa na mguu uliovunjika. Teta alikamatwa na polisi, lakini aliachiwa baada ya Weasel kuamua kutofungua mashtaka dhidi yake.

Read More
 Chameleone adokeza mpango wa kubuni bendi ya muziki ya familia

Chameleone adokeza mpango wa kubuni bendi ya muziki ya familia

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amefichua mpango wa kuunda bendi ya familia itakayojumuisha ndugu zake, Pallaso na Weasel. Katika mahojiano hivi karibuni, Chameleone ameeleza kuwa watatu hao bado wapo kwenye mazungumzo kwa ajili ya kufikia makubaliano. Bendi hiyo huenda ikazinduliwa hivi karibuni katika hafla itakayofanyika jijini Kampala, katika uwanja wa Namboole. “Tunapanga kuanzisha bendi ya familia na tutatoa mweelekeo hivi karibuni. Uzinduzi huo unahitaji ukumbi mkubwa ambao hauko tayari kwa sasa. Tunataka eneo ambalo linaweza kuchukua zaidi ya watu 40, 000,” alisema. Jose Chameleone ameweka wazi hayo kwenye mkao na waandishi wa habari wakati akielezea mipango yake juu  tamasha lake “Gwanga Mujje” litakalofanyika huko Lugogo Cricket Oval mwezi Februari mwaka huu.

Read More
 SANDRA AMTAKA DANIELLA ATIM KUTOINGILIA NDOA YAKE NA WEASEL

SANDRA AMTAKA DANIELLA ATIM KUTOINGILIA NDOA YAKE NA WEASEL

Baby mama wa msanii Weasel, Sandra Teta amemtaka mke wa Jose Chameleone’, Daniella Atim akome kuingilia masuala ya mahusiano yake. Daniella Atim amekuwa akiendesha kampeini ya kutaka haki itendeke kwa sandra teta ambaye aliripotiwa kushushiwa kipigo cha mbwa na mume wake Weasel manizo. Lakini Sandra ameonekana kutopendezwa na kitendo cha Daniella kumtetea kwenye mitandao ya kijamii kwa kusema kwamba aache kufuatilia maisha yake ya ndoa na badala ashughulike na familia yake. Hata hivyo Daniella Atim kupitia ukurasa wake wa Instagram amemjibu Sandra kwa kusema kwamba aache kujifanya ilhali anaumia moyoni kutokana na kichapo alichopewa na baby daddy wake Weasel Manizo. Daniella ameenda mbali zaidi na kusema kwamba anaelewa sandra bado anapitia kipindi kigumu katika maisha yake, hivyo anapaswa kusaidiwa kimawazo ili arejee katika hali yake ya kawaida.

Read More
 NINA ROZ AAHIDI KUMSAIDIA WEASEL KUONDOKANA NA URAIBU WA DAWA ZA KULEVYA

NINA ROZ AAHIDI KUMSAIDIA WEASEL KUONDOKANA NA URAIBU WA DAWA ZA KULEVYA

Msanii kutoka Uganda Nina Roz amehapa kumsaidia msanii mwenzake Weasel Manizo kuondokana na uraibu wa dawa za kulevya. Katika mahojiano yake Roz amesema ana uhusiano mzuri na msanii huyo hivyo ana mpango wa kuanza mazungumzo naye ili aweze kuacha kabisa kutumia dawa za kulevya na arudi tena kujishughulisha na masuala ya muziki. Mrembo huyo amedai vitendo vya Weasel kumnyanyasa kijinsia baby mama wake Sandra inatokana na msanii huyo kutumia mihadarati kupindukia. Utakumbuka Nina Roz alikuwa muathiriwa wa dawa za kulevya lakini baada ya kupelekewa kwenye kituo cha kurekebisha tabia ya waraibu wa mihadarati aliweza kuacha kutumia dawa hizo na kuamua kuokoka hivyo amekuwa akitumia muda wake mwingi kanisani akihubiri injili.

Read More