Weasel Afichua Sababu ya Kuachana na Sugar Mamas

Weasel Afichua Sababu ya Kuachana na Sugar Mamas

Mwanamuziki maarufu Weasel amefichua wazi kuwa licha ya kuwa na historia ndefu ya uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengi, hataki tena kuhusishwa na wanawake wakubwa kiumri wenye pesa maarufu kama sugar mamas. Katika mahojiano ya hivi karibuni, msanii huyo alikiri kuwa aliwahi kuchumbiana na city cougars kwa kipindi fulani, lakini sasa ameamua kuachana kabisa nao kwa kile alichokitaja kuwa ni uhusiano usio na tija. “Sikuwahi kufaidika chochote cha maana kutoka kwa mahusiano niliyokuwa nayo na sugar mamas. Ni kupoteza muda tu. Hawachangii maendeleo yoyote ya kweli kama watu wanavyodhani,” alisema Weasel. Msanii huyo kutoka Uganda alisisitiza kuwa sasa ameamua kumakinika kwenye familia yake, hasa mahusiano yake na mama wa watoto wake, Sandra Teta, ambaye kwa sasa ndiye kipenzi chake pekee. “Niliwahi kutoka na sugar mamas, lakini niliwacha. Sasa akili yangu yote iko kwa Sandra na watoto wetu. Hapo ndipo moyo wangu uko,” aliongeza. Weasel pia aliwaonya wasanii wenzake dhidi ya kuvutiwa na maisha ya mapenzi na sugar mamas, akiwashauri wawe na malengo ya muda mrefu na kuweka bidii katika kazi zao. “Wasanii wengi hupotea njia kwa sababu ya tamaa. Badala ya kujijenga kwenye muziki, wanajikuta wamelala na wanawake wenye umri mkubwa wanaowapotezea muda,” alionya. Kauli ya Weasel imepokewa kwa hisia tofauti mtandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimpongeza kwa hatua hiyo ya kimaamuzi, huku wengine wakimshangaa kutokana na historia yake ya mapenzi yenye utata. Hata hivyo, Weasel anaonekana kuwa katika njia mpya ya maisha, akiwa na mtazamo wa kutulia na kuzingatia familia na kazi.

Read More
 Mwanamuziki Weasel Manizo afunguka tusiyoyajua kuhusu Marehemu Mowzey Radio

Mwanamuziki Weasel Manizo afunguka tusiyoyajua kuhusu Marehemu Mowzey Radio

Msanii Weasel amefunguka anachokikosa kwa aliyekuwa mshirika wake kimuziki marehemu Mowzey Radio. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema kando na muziki huwa anaumia sana akimkumbuka maisha ya Radio kipindi cha uhai wake kwani walipenda sana kula bata pamoja kwenye maeneo mbali mbali ya burudani Jijini Kampala. Msanii huyo amesema ikitokea amemjua aliyehusika na mauji ya Radio hatokuja kulipiza kisasi kwani ameamua kusahau kila kitu kama njia ya kupona na maumivu aliyoyapata kutokana na kifo cha msanii huyo. Utakumbuka Mozey Radio alifariki dunia Februari 1 mwaka wa 2018 katika hospitali ya Case nchini Uganda kufuatia majeraha mabaya aliyoyapata alipovamiwa na mlinzi wa eneo moja la burudani viungani mwa jiji la Kampala.

Read More
 WEASEL MANIZO AWACHANA WANAOMKOSOA MTANDAONI KWA KUMPIGA MKE WAKE

WEASEL MANIZO AWACHANA WANAOMKOSOA MTANDAONI KWA KUMPIGA MKE WAKE

Mwanamuziki Weasel Manizo amefunguka kwa mara ya kwanza baada taarifa za kumshushia kipigo cha mbwa mke wake Sandra Teta kusambaa mtandaoni. Akizungumzia tukio hilo, Weasel amekanusha vikali tuhuma za kumpiga mke wake kwa kusema kwamba hahitaji msaada wa mtu yeyote katika kuitunza familia yake. Haikushia hapo ameenda mbali na kusema kwamba ni jambo la kushangaza kuona watu wanamkosoa mtandaoni ilhali wana migogoro katika familia zao. “Karibu kila familia ina matatizo, mbona unanizungumzia mimi kana kwamba unanijali kuliko mimi? Ninaishi maisha bora na mke wangu na sihitaji msaada wa mtu yeyote katika masuala kama haya. Geuza nguvu zako kwenye mambo mengine,” ameelezea akiwa kwenye moja ya shoo yake usiku wa kuamkia leo. Duru za kumianika zinadai kuwa wazazi wa Sandra Teta walisafiri kutoka Rwanda hadi Uganda kwa ajili ya kumuokoa binti yao kutokana na manyanyaso aliyokuwa anapitia kwenye ndoa yake.

Read More
 WEASEL MANIZO HATIANI KWA TUHUMA ZA KUMPIGA DEJAAY

WEASEL MANIZO HATIANI KWA TUHUMA ZA KUMPIGA DEJAAY

Mwanamuziki kutoka Uganda Weasel Manizo anajulikuna kuwa ni mtu mwenye hasira sana ameripotiwa kumpiga na kumjeruhi vibaya aliyekuwa dj wa kundi la Goodlyfe crew dj Triangle kwenye klabu moja ya usiku viungani mwa jiji la Kampala. Kulingana na chanzo cha karibu na msanii huyo Weasel alianza kumshushia kichapo DJ Triangle baada ya kuingia kwenye ugomvi kabla ya kupata usaidizi kutoka kwa walinzi wake. Hata hivyo maafisa wa polisi wameanzisha msako wa kumtafuta Weasel ambaye baada ya tukio hilo alisepa na timu yake mafichoni. Utakumbuka Mwaka jana Weasel alitimukia mafichoni baada ya kumpiga mfanyikazi wake wa nyumbani na kumuacha majeraha mabaya huko Neverland Makindye nchini Uganda.

Read More
 WEASEL MANIZO AWAJIBU WANAOTAKA AACHIE NYIMBO MPYA

WEASEL MANIZO AWAJIBU WANAOTAKA AACHIE NYIMBO MPYA

Mwanamuziki wa Goodlife Crew, Weasel Manizo amewatolea uvivu mashabiki zake wanaomshinikiza kila mara kuachia nyimbo mpya. Katika mkao na wanahabari Weasel amesema kwa sasa hataki kusikia mambo ya muziki na hana mpango kabisa  wa kwenda studio kurekodi nyimbo mpya kwani amejikita zaidi kwenye suala la kuiburudisha nafsi yake. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Bread & Butter” amesema pia hana mpango wa kuja na tamasha la muziki ambapo amewataka mashabiki zake wawasapoti wasanii ambao tayari wameshatangaza kufanya matamasha yao ndani ya mwaka huu. Hata hivyo hajabainika nini hasa kimepelekea msanii huyo kuzungumza hayo ila wajuzi wa mambo nchini uganda wamedai kuwa weasel hajawahi rejea katika hali yake ya kawaida tangu msanii mwenzake Radio afariki mwaka wa 2018.

Read More
 CHIKE AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA JUU YA TUHUMA ZA KUTUMBUIZA WIMBO WA RADIO & WEASEL BILA IDHINI

CHIKE AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA JUU YA TUHUMA ZA KUTUMBUIZA WIMBO WA RADIO & WEASEL BILA IDHINI

Mwanamuziki kutoka Nigeria Chike amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya msanii Weasel Manizo kumchana kwa hatua ya kuimba wimbo wa Radio na Weasel uitwao “Breath Away” kwenye moja ya performance yake wiki iliyopita. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Chike amesema hakuwa na nia ya kumvunjia heshima Weasel au mtu yeyote ila alikuwa ni njia ya kutoa heshima zake kwa marehemu Mozey Radio ambaye alikuwa mmoja kati ya wasanii  walioacha alama kwenye muziki wa Afrika. Hata hivyo chanzo cha karibu na Weasel kimesema msanii huyo ana mpango wa kuelekea mahakamani kuwafungulia mashtaka waandaji wa show yChike kwa hatua ya kumruhusu msanii huyo wa Nigeria kutumbuiza wimbo wa Radio & Weseal bila ridhaa yao.

Read More
 WEASEL MANIZO AWACHANA MAPROMOTA WA MUZIKI NCHINI UGANDA

WEASEL MANIZO AWACHANA MAPROMOTA WA MUZIKI NCHINI UGANDA

Mwanamuziki nchini Uganda Weasel Manizo amewajia juu mapromota wa muziki nchini humo mara baada ya mwanamuziki wa Nigeria Chike kuimba wimbo wake na Mozey Radio uitwao “Breath Away” kwenye moja ya performance yake bila idhini. Kupitia ukurasa wake wa Facebook Weasel ameonekana kutopendezwa na kitendo hicho huku akiwataka mapromota wa muziki wakome kuwaruhusu wasanii wa kimataifa kuimba nyimbo za wasanii wa ndani bila kuwashirikisha kwani hatua hiyo inashusha ubunifu na brand zao za muziki. Hata hivyo mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kumuunga mkono Weasel Manizo kwa kilio chake hicho kwa kuwataka mapromota wa muziki nchini uganda kuwapa kipau mbele wasanii ndani kwenye shows badala ya wasanii wa kimataifa ambao mara nyingi hushindwa kuwapa mashabiki burudani wanaohitaji.

Read More
 WEASEL MANIZZO MBIONI KUJA NA TAMASHA LA KILA MWAKA KUMUENZI MWENDAZAKE MOZEY RADIO

WEASEL MANIZZO MBIONI KUJA NA TAMASHA LA KILA MWAKA KUMUENZI MWENDAZAKE MOZEY RADIO

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Weasel Manizo ameweka wazi mpango wa kuja na tamasha la kila mwaka kwa ajili ya kumpa heshima marehemu Mozey Radio. Msanii huyo ambaye alikuwa mwanakikundi wa Goodlyfe Entertainment, amesema tamasha hilo litaitwa Radio Festival na litaanza mapema mwaka wa 2022. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamemjia juu baada ya msanii huyo kususia kuhudhuria maombi ya kumkumbuka marehemu Radio wiki iliyopita wakimtaja kuwa mnafiki kwa kushindwa kuendeleza nyayo za mozey radio kwenye tasnia ya muziki nchini  Uganda. Duru za kuaminika zinasema Weasel Manizo alisusia maombi kutokana na tofauti walizonazo na Familia ya Mozey Radio kuhusu mirabaha ya muziki wa Radio. Utakumbuka Mozey Radio ambaye alikuwa anaunda kundi la Goodlyfe alifariki mwezi Februari mwaka wa 2018 baada ya kuingia kwenye ugomvi na mlinzi wa night club moja huko Kampala uganda.

Read More
 WEASEL AFUNGUKA KWA MARA KWANZA KUHUSU KUMPIGA MFANYIKAZI WAKE WA NYUMBANI

WEASEL AFUNGUKA KWA MARA KWANZA KUHUSU KUMPIGA MFANYIKAZI WAKE WA NYUMBANI

Mwanamuziki kutoka Uganda Douglas Mayanja maarufu kama Weasel Manizo kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya kile kilichotokea kati yake na mfanyikazi wake wa nyumbani ambaye aliripotiwa kupigwa na msanii huyo. Akiwa kwenye moja ya Interview, Weasel amekanusha kumshushia kichapo mfanyikazi wake wa nyumbani huku akisema kwamba alisikia uvumi huo kutoka kwa vyombo vya habari na majukwaa mengine. Hitmaker huyo wa “Magnetic” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa vyombo vya habari vilirusha taarifa hiyo bila kujua kiini cha kupigwa kwa mfanyikazi wake wa nyumbani. Hata hivyo amesema licha ya mfanyikazi wake wa nyumbani kueleza upande wake wa stori,anasubiri apate nafuu ili aweze kuweka wazi kilichotokea kati yao kwa kina.

Read More