Weezdom Amkosoa Bahati kwa Kuvaa Mavazi ya Mkewe
Msanii wa zamani wa muziki wa injili na meneja wa burudani, Weezdom, ameeleza masikitiko yake kuhusu mwenendo wa msanii Bahati, ambaye kwa sasa amegeukia maudhui yenye utata mtandaoni. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram, Weezdom amesema Bahati alikuwa mfano bora wa kuigwa, hasa kwa vijana na familia, na aliwahi kutumia kipaji chake kueneza neno la Mungu kupitia muziki. Lakini sasa anahisi kuwa Bahati amepoteza dira na kusahau msingi wa mafanikio yake. “Sometimes naangalia vitu my mentor, msee mwenye alinifunza Word ya God, vitu anafanya kwa mitandao namhurumia sana. Juu hakuna brand ilishawahi kuwa na influence kubwa kwa wazazi na watoto wadogo zaidi ya huyu jamaa bana!” aliandika Weezdom kwa hisia. Weezdom, ambaye aliwahi kuwa mshirika wa karibu wa Bahati katika huduma ya muziki wa injili, aliongeza kuwa Bahati anapaswa kutafakari upya nafasi yake kama kielelezo kwa vijana na kurejea kwenye msingi wa kiimani uliomuinua kimaisha. Kauli hiyo inakuja baada ya video na picha za Bahati kusambaa mitandaoni zikimwonyesha akiwa amevaa nguo za mkewe, jambo lililoibua maoni mseto kutoka kwa mashabiki na wafuasi wake. Ujumbe wa Weezdom umechochea mijadala mikubwa mitandaoni, wengi wakijiuliza iwapo Bahati anapaswa kurejea kwenye muziki wa injili au kuendelea na mwelekeo wake wa sasa wa burudani mchanganyiko. Mpaka sasa, Bahati hajatoa tamko lolote rasmi kujibu maoni ya Weezdom, lakini mashabiki wengi wanaendelea kuonyesha maoni yao tofauti kuhusu suala hilo, baadhi wakimtetea na wengine wakimtaka arejee kwenye msingi uliompa umaarufu.
Read More