Mwigizaji Wilbroda Asema Haamini Kuwepo kwa Mbingu na Jehanamu Baada ya Kifo.
Mwigizaji maarufu wa Kenya, Jacquey Nyaminde, anayejulikana zaidi kwa jina lake la uigizaji Wilbroda, ameibua mjadala baada ya kufichua mtazamo wake kuhusu imani ya maisha baada ya kifo. Akizungumza na Podcast ya Mwakideu Live, Wilbroda amesema kuwa haamini kuwepo kwa mbingu na jehanamu, akiongeza kuwa hakuna siku tarumbeta itapigwa kama inavyoaminika katika mafundisho ya dini. Kauli yake imezua hisia mseto miongoni mwa mashabiki na wafuasi wake, wengine wakiheshimu msimamo wake binafsi huku wengine wakikosoa mitazamo hiyo ikizingatiwa kuwa masuala ya kiimani ni nyeti kwa jamii nyingi. Wilbroda, ambaye amejulikana kwa muda mrefu kupitia kipindi cha Papa Shirandula na kazi yake katika uigizaji wa vichekesho, amesema mara kadhaa kwamba maisha yake ya kiroho ni safari ya kibinafsi, na kila mtu anapaswa kuwa huru kuchagua kile anachoamini.
Read More