WILL SMITH APATA OFA NYINGI ZA KUIGIZA FILAMU MAREKANI

WILL SMITH APATA OFA NYINGI ZA KUIGIZA FILAMU MAREKANI

Mwigizaji kutoka nchini Marekani Will Smith ameripotiwa kupata ofa nyingi za kuigiza filamu mbalimbali licha ya kufungiwa miaka 10 kuhudhuria kwenye hafla yoyote ile ya Oscars. Kwa mujibu wa Jarida la Daily Star, Smith amepata ofa nyingi za kuigiza na tayari makampuni mengi ya kustream filamu yanafanya jitihada za kufanya nae kazi tangu tukio lake la kumpiga kibao mchekeshaji Chris Rock wakiwa jukwaani kwenye hafla ya tuzo za Oscars. Tukio hilo la Will Smith limeonekana kutoathiri kabisa kazi zake za filamu, licha ya wengi kudhania kwamba lingeweza kumnyima baadhi ya dili mbalimbali.

Read More
 WILL SMITH YUPO ‘REHAB’ AANZA KUPATIWA MSAADA WA KITAALAMU

WILL SMITH YUPO ‘REHAB’ AANZA KUPATIWA MSAADA WA KITAALAMU

Mwigizaji kutoka Marekani Will Smith ameripotiwa kuwa yupo kituo cha kupokea matibabu ya Kisaikolojia (Rehab). Tovuti ya Hollywood Insiders imeliambia gazeti la The Sun kwamba mwigizaji huyo amefika kwenye kituo hicho na atakuwa akipatiwa msaada namna ya kupambana na msongo wa mawazo. “He will be getting help on dealing with stress… this is unquestionably the battle of his career” – chanzo cha karibu na Smith kimeliambia The Sun. Haya yanajiri ikiwa ni wiki chache zimepita kufuatia tukio la kumchapa kibao jukwaani mchekeshaji Chris Rock kwenye hafla ya Tuzo za Oscars, 2022.

Read More
 WILL SMITH AFUNGIWA MIAKA 10 KUSHIRIKI TUZO ZA OSCAR

WILL SMITH AFUNGIWA MIAKA 10 KUSHIRIKI TUZO ZA OSCAR

Hatimaye Mwigizaji Will Smith hatoruhusiwa kuhudhuria Tuzo za Oscar kwa miaka 10 kutoka sasa ikiwa ni adhabu baada ya kumpiga kibao Mchekeshaji Chris Rock jukwaani wakati wa Tuzo hizo za mwaka huu. Smith hatoruhusiwa kuhudhuria hafla au programu zozote za Academy, yeye binafsi au hata kwa mtandao. Lakini pia barua hiyo imeeleza shukrani nyingi kwa Chris Rock kwa utulivu wake wakati wa hali isiyo ya kawaida. Hata hivyo, baada ya marufuku hii ya miaka 10 Will Smith ameonesha kukubali adhabu aliyopewa kwa kuiambia CNN kwamba anakubali na kuheshimu uamuzi huo.

Read More
 WILL SMITH AMUOMBA CHRIS ROCK MSAMAHA KWA MARA YA PILI

WILL SMITH AMUOMBA CHRIS ROCK MSAMAHA KWA MARA YA PILI

Mwanamuziki na mwiigizaji kutoka Marekani Will Smith amemuomba radhi mchekeshaji Chris Rock pamoja na watayarishaji wa Tuzo za Oscars kufuatia tukio la kumchapa kofi mchekeshaji huyo live Jukwaani wakati wa ugawaji wa Tuzo hizo za 94 usiku wa kuamkia Machi 28, katika ukumbi wa Dolby Theatre, Hollywood nchini Marekani. Will Smith ambaye tayari aliomba radhi akiwa Jukwaani punde baada ya kitendo kile, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameomba radhi tena kwa kusema kitendo kile hakikubaliki kwa namna yoyote. Mwiigizaji huyo amesema anapokea utani wa aina yoyote lakini utani juu ya mke wake Jada Pinkett  na afya yake alishindwa kuuvumilia. “Ningependa mbele ya Umma kukuomba radhi Chris Rock, nilikuwa nje ya mstari na nilikosea. Nimejifedhehesha, na vitendo vyangu havikuwa dira au mfano wa Mwanaume ambaye natakuwa kuwa. Hakuna nafasi ya vurugu kwenye hii dunia ya upendo na ukarimu. Pia naomba radhi kwa Academy na watayarishaji wa show, wahudhuriaji wote na watazamaji.” aliandika Will Smith na kumalizia kuwa anajutia kwa kitendo kile. Aidha, imeripotiwa kwamba usimamizi wa tuzo za Oscar unaandaa mkutano wa dharura kuamua hatua zitakazochukuliwa dhidi ya Will Smith

Read More
 WILL SMITH AMSHUSHIA KICHAPO CHA MBWA MCHEKESHAJI CHRIS ROCK LIVE JUKWAANI KWENYE TUZO ZA OSCARS

WILL SMITH AMSHUSHIA KICHAPO CHA MBWA MCHEKESHAJI CHRIS ROCK LIVE JUKWAANI KWENYE TUZO ZA OSCARS

Mwiigizaji na mwanamuziki kutoka Marekani Will Smith ametawala vichwa vya habari duniani asubuhi hii baada ya kumshushia kichapo mchekeshaji Chris Rock live Jukwaani wakati wa ugawaji wa Tuzo za Oscars. Chris Rock alifanya utani juu ya mke wa Will Smith, Jada Pinkett ndipo Will Smith aliamka na kupanda Jukwaani ambapo alimchapa kofi la nguvu mchekeshaji huyo na kumwambia mara mbili “Keep my wife’s name out of your f-cking mouth.” Baadaye Will Smith alipanda Jukwaani baada ya kushinda Tuzo ya Best Actor ambapo kwenye hotuba yake alisema alifanya kitendo hicho kwa lengo la kulinda familia yake dhidi ya chochote. Hata hivyo aliishia kuomba radhi mbele ya wahudhuriaji na kila mmoja aliyekuwa akitazama tuzo za Oscar kupitia runinga.

Read More