Wily Paul Aanikwa na Martina kwa Kumsumbua kwenye DM
Mrembo na mwana mitandao kutoka Kenya, Martina, amezua gumzo mtandaoni baada ya kufichua kuwa msanii Wily Paul, ndiye staa ambaye amekuwa akimvizia kwenye DM kwa muda mrefu. Akipiga stori na kipindi cha Feast with Friends, Martina alijibu swali la mtangazaji aliyetaka kujua ni staa gani wa kiume ambaye amekuwa akijaribu kumtongoza au kumpigia mistari ya kimahaba kwenye DM. Bila kusita, alitaja jina la Wily Paul, akidai kwamba ameendelea kumwandikia jumbe mara kwa mara bila mafanikio. “Sitajificha, ni Wily Paul. Amekuwa akiniandikia sana kwa muda mrefu lakini sijawahi kumjibu. Nimekuwa nikipuuza tu,” alieleza Martina huku akicheka kwa aibu. Kauli hiyo imeibua hisia mseto mitandaoni. Baadhi ya mashabiki walihoji kama Martina alikuwa anatafuta kiki, huku wengine wakisema kauli hiyo inaakisi tabia ya msanii huyo ambaye amekuwa akiandamwa na madai ya kuhusika na skendo mbalimbali za kimapenzi. Wily Paul bado hajatoa tamko rasmi kuhusiana na tuhuma hizo, lakini hii si mara ya kwanza msanii huyo kuhusishwa na skendo za kimapenzi na influencers maarufu mitandaoni.
Read More