WIZ KHALIFA AWAPA SOMO MARAPA MAREKANI KUFUATIA MAUJI YA KIHOLELA
Rapa kutoka nchini Marekani Wiz Khalifa ametaka heshima iwepo kwenye muziki wa Hiphop ambapo amewaonya Mastaa wenzake kujitenga na vurugu kuelekea Mwaka mpya kutokana na vifo vya maRapa Drakeo The Ruler na Young dolph Wiz Khalifa ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake Wa Twitter kwa kuandika ujumbe unaosomeka “Kama waburudishaji tujaribu kitu kipya mwaka ujao. Tujali mambo yetu binafsi, tusidharauliane familia zetu, wafu, au mahali mtu anakotoka.” Haikushia hapo mkali huyo wa ngoma ya “See You Again” ameenda mbali zaidi na kusema kwamba “Tusichukulie madhaifu ya mtu kumweka chini na kumjia juu. Tuoneshe upendo ambao wewe binafsi unatarajia kupata kutoka kwa wengine” Wiz Khalifa amewashauri Marapa wa muziki wa hiphop nchini Marekani kuacha kufuatana na makundi yenye tabia za kihalifu ambapo amewarai waache tabia ya kuposti mambo yao ya faragha mitandaoni. Ikumbukwe Wasanii wakongwe mbalimbali nchini Marekani wakiwemo The Game, Maino na Fat Joe wamejitokeza kutoa ushauri kwa wasanii wa sasa kufuatia mauji ya Marapa yanayoendelea nchini humo ambapo mpaka sasa zaidi ya Marapa 10 wameuwawa.
Read More