Pendekezo la Timu 64 Katika Kombe la Dunia 2030 Lateka Vichwa vya Habari

Pendekezo la Timu 64 Katika Kombe la Dunia 2030 Lateka Vichwa vya Habari

Suala la kuongeza idadi ya timu shiriki katika fainali za Kombe la Dunia hadi kufikia 64 limeibuka tena, kufuatia kikao kati ya maafisa wakuu wa CONMEBOL shirikisho la soka la Amerika Kusini na uongozi wa FIFA, ambapo pendekezo hilo liliwasilishwa rasmi kwa ajili ya michuano ya mwaka 2030. Kwa sasa, Kombe la Dunia la mwaka 2026 tayari limepangwa kushirikisha timu 48, lakini CONMEBOL inaamini kuwa wakati umefika wa kuongeza tena idadi hiyo hadi timu 64, ili kutoa fursa kwa mataifa mengi zaidi kushiriki katika tamasha hilo kubwa la kandanda duniani. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, pendekezo hilo liliwasilishwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa baraza la FIFA mwezi Machi, na kuungwa mkono na Ignacio Alonso, rais wa shirikisho la soka la Uruguay. Alonso alisisitiza kuwa hatua hiyo itaongeza ushindani na kuifanya michuano hiyo kuwa ya kipekee kwa maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Kombe la Dunia. Fainali za mwaka 2030, ambazo ni za kihistoria kwa kuwa ni karne moja tangu fainali za kwanza kuandaliwa mwaka 1930 nchini Uruguay, zimepangwa kufanyika kwa ushirikiano wa Uhispania, Ureno na Morocco. CONMEBOL inatumai kuwa kwa kuwa wenyeji watakuwa zaidi ya mmoja, ongezeko la timu litaleta uwiano wa kisiasa, kijiografia na kiushindani katika mashindano hayo. Kwa muktadha wa kihistoria, idadi ya timu katika Kombe la Dunia imekuwa ikiongezeka kadri muda unavyosonga. Mwaka 1982, idadi ya timu iliongezwa hadi 24, na kisha 32 mwaka 1998. Ongezeko la sasa kutoka 48 hadi 64 linaonekana kuwa hatua inayofuata kiasili, hasa kwa kuzingatia ongezeko la mataifa wanachama wa FIFA na ubora unaoendelea kuongezeka duniani kote.

Read More
 ARSENE WENGER ASEMA KUNA UWEZEKANO WA OFFSIDE KUAMULIWA NA TEKNOLOJIA MWAKA 2022

ARSENE WENGER ASEMA KUNA UWEZEKANO WA OFFSIDE KUAMULIWA NA TEKNOLOJIA MWAKA 2022

Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuna uwezekano mkubwa kwamba maamuzi ya ‘Offside’ yakaamuliwa moja kwa moja kwa kutumia Teknolojia kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 zitakazofanyika nchini Qatar. Wenger ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa maendeleo ya mpira wa miguu katika Shirikisho la Soka duniani FIFA, amesema hiyo itakuwa hatua kubwa kwenye soka la dunia kwani pia itapunguza lawana nyingi kwa waamuzi. Kwa sasa teknolojia imechukua nafasi kubwa kwenye mpira kwani maaumizi mengi nyeti yanafanywa na VAR na Goal Line Technology.

Read More