Wyre, Nameless na Jua Cali kutengeneza bendi ya muziki

Wyre, Nameless na Jua Cali kutengeneza bendi ya muziki

Msanii mkongwe nchini, Wyre amedokeza mpango wa kuunda bendi ya muziki itakayojumuisha wasanii wa kizazi kipya pamoja na wa zamani. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, amepost video akitoa tangazo hilo ambapo amesema wameungana na kutengeneza timu ya malejendari wa muziki. “Kuna nini jamani. Kwa kawaida sifanyi hivi. Imekuwa zaidi ya miaka 20 katika kufanya jambo hili la muziki na nadhani ni kuhusu wakati huu ambao umefika…. Unajua kila kitu kinafikia hatua hiyo ya kufika mwisho. “Kwa hivyo nimeamua.. Tumeamua kuwa tunaunda bendi ya wasanii wa kitambo,” Msanii huyo aliweka wazi hilo huku akihamishia kamera kwa wasanii wengine ambao ni Nameless na Jua Calie pamoja na Kenzo.

Read More
 NECCESARY NOIZE WATANGAZA UJIO MPYA BAADA YA KIMYA CHA MUDA MREFU

NECCESARY NOIZE WATANGAZA UJIO MPYA BAADA YA KIMYA CHA MUDA MREFU

Wanamuziki nazizi na wyre wametangaza marejeo ya kundi lao la muziki Necessary Noize. Nazizi kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza ujio wa EP yao mpya yenye nyimbo 8 za moto ambayo itaingia sokoni Mei 5 mwaka huu na kazi hiyo itapatikana pia kwenye majukwaa ya mitandaoni kama vile Spotify. Nazizi amesema wamechukua muda mrefu kuachia EP hiyo kwa sababu walikuwa wameshikaka na majukumu mengine ya kibinafsi. Kundi la muziki la Necessary Noize lilianzishwa mwaka 2000 na nazizi na wyre. Album yao ya kwanza ilitoka mwaka huo huo wa 2000, ilikuwa na nyimbo kama vile “Clang Clang” na “La Di Da.” Album ya pili ya Necessary Noize iliyoitwa Necessary Noize II: Kenyan Gal, Kenyan Boy ilitoka mwaka 2004 na ilikuwa na nyimbo maarufu kama vile “Kenyan Gal, Kenyan Boy” na “Bless My Room.

Read More
 WYRE AWATAKA WASANII KUJIUNGA NA BODI ZA MUZIKI KENYA

WYRE AWATAKA WASANII KUJIUNGA NA BODI ZA MUZIKI KENYA

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Kenya Wyre ametoa changamoto kwa wasanii wenzake kujiunga na bodi zinazojihusisha na muziki ili kuleta mabadiliko kwenye tasnia ya muziki nchini humo. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Wyre amesema inasikitisha kuona wasanii wa muziki nchini Kenya wanapinga utendakazi wa bodi za muziki nchini humo wakati sio wanachama wa bodi hizo jambo ambalo anadai imekuwa vigumu kwao kutekeleza baadhi ya mabadiliko wanayotaka kwenye tasnia ya muziki. Mbali na hayo Wyre amezindua jukwaa lake la muziki liitwalo Blow Africa litakalo toa fursa kwa wasanii chipukizi kuingiza kipato kupitia kazi zao za muziki. Wyre amesema kwa kipindi cha miezi minane amekuwa akifanya kazi jukwaa hilo kwa ushikiriano na baadhi ya wadau wa maendeleo kuhakikisha wasanii wanaboreka kiuchumi.

Read More