Real Madrid Yamtambulisha Rasmi Xabi Alonso Kuwa Kocha Mpya
Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania imemtambulisha rasmi Xabi Alonso kuwa kocha mpya wa kikosi hicho, ambapo ataanza kazi yake kuanzia msimu wa 2025/2026. Alonso amesaini mkataba wa miaka mitatu ambao utamuweka klabuni hadi mwaka 2028. Xabi Alonso mwenye umri wa miaka 43 anarejea tena Real Madrid, safari hii kama kocha, baada ya kuichezea timu hiyo kati ya mwaka 2009 hadi 2014. Akiwa mchezaji wa Real Madrid, alishinda mataji mbalimbali kabla ya kuhamia klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani. Uongozi wa Real Madrid umeeleza kuwa unamatumaini makubwa kwa Alonso kutokana na mafanikio aliyoyapata akiwa kocha wa Bayer Leverkusen, ambapo alionyesha uwezo mkubwa wa kiufundi. Mashabiki wa Real Madrid sasa wanatarajia kuona mafanikio mapya chini ya uongozi wa nyota wao wa zamani
Read More