Nandy Asikitishwa na Taarifa za Yammi, Aomba Faragha na Heshima

Nandy Asikitishwa na Taarifa za Yammi, Aomba Faragha na Heshima

Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Nandy, amepatwa na kigugumizi kuzungumzia taarifa zilizogonga vichwa vya habari kwamba msanii wake wa zamani Yammi alifikiria kujiua kutokana na msongo wa mawazo. Katika mahojiano maalum na waandishi wa habari, Nandy amesema kuwa taarifa hizo zilimshtua na kumgusa sana, na kwamba anatamani kukutana na Yammi uso kwa uso ili wazungumze kwa kina, badala ya kuwasiliana kwa njia ya simu pekee. Hata hivyo, Nandy ametumia fursa hiyo kuwaomba waandishi wa habari kuacha kumuliza maswali kuhusu Yammi kila mara anapofanya mahojiano. Amesema hatua hiyo imekuwa ikimletea usumbufu wa kihisia na kuonekana kama chanzo cha matatizo ya hitmaker huyo wa ngoma ya “Raha”. Tamko hilo la Nandy limekuja wakati mashabiki wengi wakiendelea kutoa maoni tofauti kuhusu uhusiano wa wawili hao, huku baadhi wakihusisha tofauti zao na suala la Yammi kuwa msanii aliyekuwa chini ya lebo ya The African Princess inayomilikiwa na Nandy kabla ya kuondoka kimyakimya

Read More
 “Bora Nife Nikapumzike…” – Yamii Aandika Ujumbe wa Kushtua Instagram

“Bora Nife Nikapumzike…” – Yamii Aandika Ujumbe wa Kushtua Instagram

Msanii chipukizi wa muziki wa Bongo, Yamii, ameibua hofu mitandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kusikitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram akieleza hali ya kukata tamaa na msongo wa mawazo, kabla ya kuufuta muda mfupi baadaye. Katika ujumbe huo, Yamii alielezea hali ya kuchoka kimaisha na kusema kuwa haoni tena sababu ya kuendelea kuishi, akionesha kuwa amefikia kikomo cha uvumilivu wake. Aliomba msamaha kwa wazazi wake, ndugu na mashabiki, akionekana kubeba huzuni kubwa moyoni. Aliitaja pia msanii mwenzake Nandy, akimwomba radhi iwapo aliwahi kumkosea. “Mashabiki zangu naombeni mniombee. Msamaha kwa mama angu na baba angu na baba yangu. Mimi ndio tegemeo lakini naona siwezi kuishi tena. Nimechoka, bora nife nikapumzike. Naombeni msamaha kwa wote wote niliowahi kuwakosea. Mimi basi tena nimefika mwisho, siwezi tena, bora nikapumzike. Siwezi tena siwezi tena walahi siwezi… @officialnandy pia dada angu naomba nisamehe popote niliwahi kukukosea,” Aliandika kwa hisia kali Ujumbe huo ulisambaa kwa kasi mitandaoni, huku mashabiki na watu maarufu wakieleza kusikitishwa na hali hiyo. Wengi walihoji hali ya afya ya kiakili ya msanii huyo na kutoa wito kwa watu wa karibu naye kumsaidia haraka. Baada ya ujumbe huo kufutwa, mjadala uliendelea kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya mashabiki wakianza kampeni ya kumwombea na kumtia moyo kwa hashtag kama #PrayForYamii na #MentalHealthMatters. Wengine walitoa wito kwa wasanii wenzake, familia na mashabiki kuwa karibu naye ili kumsaidia kupitia kipindi hiki kigumu. Hadi kufikia sasa, Yamii hajatoa kauli yoyote rasmi kuhusu ujumbe huo, na haijafahamika hali yake ya sasa. Mashabiki na wadau wa burudani wanaendelea kufuatilia kwa makini

Read More
 Nandy Ampongeza Yammi Siku ya Kuzaliwa Licha ya Kuondoka The African Princess

Nandy Ampongeza Yammi Siku ya Kuzaliwa Licha ya Kuondoka The African Princess

Mwanamuziki nyota wa Bongofleva , Nandy, ameonyesha kuwa bado ana upendo na heshima kwa Yammi licha ya kumaliza rasmi mkataba wa kimuziki na nyota huyo wa muziki. Kupitia Insta Story kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nandy ambaye mkurugenzi wa lebo ya The African Princess amempongeza Yammi kwa siku yake ya kuzaliwa, akimtakia kheri na mafanikio katika maisha na muziki, ikiwa ni ishara ya kudumisha mahusiano mema nje ya kazi. “Happy born day msanii, keep shining @yammitz,” aliandika Nandy. Ujumbe huo umekuja wakati mashabiki wakifuatilia kwa karibu mahusiano kati ya wawili hao, kufuatia kuondoka kwa Yammi kutoka kwenye lebo hiyo aliyokuwa chini yake kwa muda na kujipatia umaarufu kupitia nyimbo kama “Namchukia” na “Tunayoyaweza”. Mapokezi ya ujumbe huo yamekuwa chanya, huku mashabiki wakisifia ukomavu wa Nandy kama kiongozi wa sanaa na mfano wa kuigwa katika kudumisha heshima hata baada ya ushirikiano wa kikazi kufikia mwisho. Hadi sasa, Yammi hajajibu hadharani ujumbe huo, lakini wengi wanatarajia kuwa hatua hiyo ni mwanzo wa ukurasa mpya wa amani na heshima kati ya wasanii hao wawili waliowahi kushirikiana kwa karibu.

Read More
 Yammi Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kuondoka The African Princess

Yammi Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kuondoka The African Princess

Msanii wa muziki wa Bongo, Yammi, ameandika ujumbe mzito wa kihisia katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa leo, ikiwa ni mara ya kwanza kujitokeza hadharani tangu kuachana na lebo ya The African Princess inayoongozwa na Nandy. Kupitia mtandao wake wa Instagram, Yammi amechapisha ujumbe wa kwanza rasmi tangu aachane na lebo hiyo, akieleza hisia zake za ndani kuhusu safari yake ya muziki, changamoto alizokutana nazo, na matumaini ya mustakabali mpya. “Leo ni wakati muhimu sana kwangu, safari yangu haijawahi kuwa rahisi. Mipaka yangu imejaribiwa kwa njia ambazo sikuweza hata kufikiria… Kuna muda nilitaka kukata tamaa, lakini kupitia yote nimegundua kuwa lazima nibaki imara na kuendelea kufuata ndoto zangu.” Aliandika Katika ujumbe huo uliogusa hisia za mashabiki wengi, Yammi alieleza kuwa kila changamoto aliyopitia imemfunza kitu na kumjenga kuwa msanii mwenye maono mapya na nguvu zaidi. “Kila sehemu na kila jambo limenifundisha vitu. Alhamdulillah… here I come more stronger and determined than ever!” Alimalizia kwa hisia kali. Mashabiki wake wamemiminika kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii wakimpongeza kwa ujasiri na kumtakia mafanikio mema katika hatua yake mpya ya maisha ya muziki. Wengi wamesisitiza kuwa wanamsubiri kwa hamu na shauku kubwa, wakiamini kuwa Yammi bado ana mengi ya kuonyesha duniani. Yammi, ambaye alifahamika kupitia vibao kama “Namchukia” na “Tunayoyaweza”, alikuwa mmoja wa wasanii waliokuwa wakikuzwa chini ya lebo ya The African Princess, inayomilikiwa na Nandy. Tangu kuingia kwake kwenye tasnia ya muziki, ameonyesha uwezo mkubwa wa sauti, hisia, na utunzi wa hali ya juu. Uamuzi wake wa kuachana na lebo hiyo bado haujaelezwa kwa kina, lakini ujumbe wake wa kihisia unaashiria mwanzo mpya na ari ya kuendelea kupambana ili kufanikisha malengo yake ya kisanii.

Read More
 Nandy amtambulisha msanii mpya ndani ya lebo yake

Nandy amtambulisha msanii mpya ndani ya lebo yake

Msanii wa Bongofleva Nandy amemtambulisha msanii mpya na wa kwanza ndani ya lebo yake ya “The African Princess”, anaitwa Yammi Nandy ambaye ndiye mkurugenzi wa “The African Princess Label”, amemtaja msanii wake mpya Yammi kuwa ni binti mdogo mwenye ndoto ya kuwa msanii mkubwa na mafanikio. Aidha,Yammi amewashukuru Watanzania kwa mapokezi yao katika safari yake ya muziki ambayo ameianza rasmi Januari 19, mwaka 2023. “Asanteni sana kwa watu wote mlionipokea vizuri. Kiukweli nina mengi ya kuwashukuru ila niseme tu Nawapenda Sana  #ThreeHearts #ItsYammi”, Yammitz ametumia ukurasa wake wa Instagram kushukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata. Yammi tayari ameachia EP yake mpya iitwayo Three hearts yenye nyimbo 3 ambazo ni Namchukia, Tunapendezana na Hanipendi. Inapatikana kupitia mitandao ya kupakua na kusikiliza muziki duniani.

Read More