BINTI WA FLYOD MAYWEATHER AKIRI KOSA LA  KUMCHOMA KISU MZAZI MWENZA WA NBA YOUNGBOY

BINTI WA FLYOD MAYWEATHER AKIRI KOSA LA KUMCHOMA KISU MZAZI MWENZA WA NBA YOUNGBOY

Binti wa Floyd Mayweather,Yaya Mayweather amekiri kuwa na hatia ya kutenda kosa la kumchoma Kisu mzazi mwenza wa Rapa NBA YoungBoy, tukio lililotokea Aprili mwaka 2020. Yaya ambaye bado anadaiwa kuwa kwenye mahusiano na NBA YoungBoy, amekiri kosa hilo mbele ya waendesha mashtaka wa mahakama ya kitongoji cha Harris mjini Houston. Kosa hilo linabeba hukumu ya kifungo cha hadi miaka 20 Jela. Waendesha mashtaka wamependekeza kwamba ahukumiwe kifungo cha nje miaka 6 ambacho hutolewa kwa wakosaji wa mara ya kwanza na pia kufanya shughuli za kijamii chini ya uangalizi.

Read More