Kanye West Aonyesha Furaha Baada ya Larry Hoover Kumpunguzia Kifungo, Atoa Shukrani kwa Drake

Kanye West Aonyesha Furaha Baada ya Larry Hoover Kumpunguzia Kifungo, Atoa Shukrani kwa Drake

Msanii maarufu wa Marekani, Ye (Kanye West), ameonyesha furaha yake baada ya Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump, kupunguza kifungo cha aliyekuwa kiongozi wa genge kutoka Chicago, Larry Hoover. Ye alionyesha shukrani kwa msanii mwenzake Drake kwa mchango wake katika juhudi za kumkomboa Hoover, akitambua ushirikiano wao kama sehemu muhimu ya mafanikio haya. “THANK YOU DRAKE FOR HELPING TO BRING LARRY HOOVER HOME.”, Aliandika X Ye na Drake waliweka tofauti zao kando na kuungana kwa tamasha la pamoja mnamo mwaka 2021, likiwa ni sehemu ya kampeni ya kumtetea Hoover na kushinikiza kuachiliwa kwake. Tamasha hilo liliitwa Free Larry Hoover Benefit Concert na lilileta msukumo mkubwa kwa umma na viongozi kuhusu kesi ya Hoover. Larry Hoover alikuwa akitumikia kifungo cha maisha kwa makosa ya uhalifu wa genge, lakini amekuwa akihusishwa na mabadiliko chanya akiwa gerezani. Uamuzi wa kupunguziwa kifungo wake umetajwa na baadhi ya watu kama hatua ya kihistoria katika juhudi za mageuzi ya mfumo wa haki nchini Marekani. Kwa Ye, huu ni ushindi mkubwa kwa familia ya Hoover na kwa wale wanaoamini katika nafasi ya pili na msamaha wa kweli.

Read More
 Ushahidi wa Kid Cudi Dhidi ya Diddy Wamvunja Moyo Kanye West

Ushahidi wa Kid Cudi Dhidi ya Diddy Wamvunja Moyo Kanye West

Rapa maarufu mwenye utata, Kanye West, ametoa hisia zake kuhusu hali inayoendelea kumkumba Sean Diddy Combs, akieleza masikitiko yake juu ya hatua ya Kid Cudi kutoa ushahidi dhidi ya Diddy. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Ye ameonekana kuzungumzia kile anachokiona kama mfumo wa haki unaowakandamiza watu weusi, akisisitiza haja ya jamii ya wasanii na Wamarekani Weusi kwa ujumla kujilinda na kushikamana badala ya kushirikiana na mifumo anayoamini kuwa ya kibaguzi. “I wish Cudi hadn’t testified against Puff. We need to not be locked in white systems. Praying for Puff and his family. Praying for Puff Daddy and the Family.”Aliandika X Kauli hiyo imeibua hisia mseto kutoka kwa mashabiki na wanamuziki wenzake, huku baadhi wakimtetea kwa msimamo wake wa kutaka mshikamano miongoni mwa wasanii wa asili ya Kiafrika, na wengine wakimkosoa kwa kudharau mchakato wa haki. Kid Cudi, ambaye zamani alikuwa rafiki wa karibu wa Ye, anatajwa kuwa miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi dhidi ya Diddy kufuatia madai mazito yanayomkabili kuhusu vitendo vya unyanyasaji na ukiukaji wa haki.

Read More
 Ye Aomba Msamaha kwa Mungu, Atangaza Kuachana na Chuki Dhidi ya Wayahudi

Ye Aomba Msamaha kwa Mungu, Atangaza Kuachana na Chuki Dhidi ya Wayahudi

Rapa mwenye utata na mabadiliko ya ghafla, Kanye West, anayejulikana pia kama Ye, ameandika ujumbe mzito wa toba kupitia mtandao wa X (zamani Twitter), akiomba msamaha kwa Mungu kwa maumivu aliyowahi kusababisha, huku akitangaza kuwa amewasamehe wote waliomuumiza. Katika ujumbe huo uliojaa hisia, Ye alisema ameacha kabisa chuki aliyokuwa nayo dhidi ya Wayahudi, na sasa anawapenda watu wote bila ubaguzi. “Nimeomba msamaha kwa Mungu. Nimewasamehe waliotenda mabaya dhidi yangu, na sasa nawafurahia wanadamu wote,” aliandika rapa huyo. Ye pia aligusia mawasiliano ya karibu na watoto wake, akieleza kuwa waliwasiliana naye kwa FaceTime tu,kio lililomgusa sana na kuonekana kuwa na nafasi maalum katika mabadiliko yake ya kiroho na kibinadamu. Ujumbe wake umezua maoni mseto miongoni mwa mashabiki. Wengine wamepokea hatua hiyo kama mwanzo mpya kwa msanii huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa matamshi yenye utata na msimamo mkali kuhusu masuala ya kidini, kisiasa na kijamii. Tangazo hili linakuja baada ya kipindi kirefu cha shutuma nzito kutokana na matamshi yake yaliyotafsiriwa kama chuki dhidi ya Wayahudi, na hata kusababisha kupoteza mikataba mikubwa ya kibiashara. Toba yake sasa imechukuliwa kama jaribio la kurejesha uhusiano na jamii na pia kurekebisha taswira yake kwa umma. Hadi sasa, ujumbe huo tayari umepata maelfu ya likes na maoni, wengi wakisubiri kuona kama mabadiliko haya ni ya kudumu au ni sehemu nyingine ya mzunguko wa tabia za Ye ambazo mara nyingi husababisha taharuki mitandaoni.

Read More