Msanii Ykee Benda mbioni kufanya show yake mwakani

Msanii Ykee Benda mbioni kufanya show yake mwakani

Nyota wa muziki kutoka nchini Uganda Ykee Benda ametangaza tarehe ambayo atafanya show yake ijayo. Kupitia mitandao yake ya kijamii Bosi huyo wa Mpaka Records amesema ana mpango wa kuindaa show yake Mei 13 mwaka 2023 ingawa hajaweka wazi eneo ambalo atafanyia show hiyo. Kwa mwaka huu,Ykee Benda ametoa nyimbo zaidi 8 ambazo zimepokelewa kwa ukubwa na mashabiki zake. Mwimbaji huyo anajiunga na wasanii kama Jose Chameleone, Spice Diana, King Saha na Karole Kasita ambao tayari wametangaza tarehe ambayo watafanya shows zao mwaka 2023. Utakumbuka 2019 Ykee Benda alipata mapokezi mazuri kwenye show yake iitwayo Singa ambayo ilifanyika Serena Hotel, jijini Kampala.

Read More
 Ykee Benda awatambulisha wasanii wa UgaBoys kwenye lebo yake ya Mpaka Records

Ykee Benda awatambulisha wasanii wa UgaBoys kwenye lebo yake ya Mpaka Records

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Ykee Benda amewatambulisha wasanii wa kundi la Ugaboys katika lebo yake ya muziki ya Mpaka Records. Katika mkao na wanahabari Ykee amesema ameingia ubia wa kufanya kazi na wasani wa UgaBoys kwa ushirikiano na lebo ya muziki yenye makazi yake nchini Norway, Sundance kwa ajili ya kutanua wigo wa muziki wa Uganda uweze kufika mbali zaidi. Lakini pia amesema tayari amekamilisha michakato ya kisheria ya kufanya kazina wasanii hao chini ya Mpaka Records huku akisema kuwa ana imani nao kwani wana vipaji vya kipekee kwenye muziki wao. Kundi la Ugaboys ambalo linaundwa na wasanii Malinga Sulaiman na Musungi Muhammmad awali walikuwa wamesainiwa chini ya lebo ya muziki ya Black Market Records lakini walikuja wakaingia kwenye ugomvi na lebo hiyo walipokwenda kinyume na mkataba wao kwa kuachia wimbo uitwao “Gimmie” waliokuwa wamemshirikisha Ykee Benda. Utakumbuka mwaka wa 2019 Ykee Benda alimsajili msanii Dre Cali kwenye lebo yake ya Mpaka Records lakini mwaka wa 2021 baada ya kupata mafanikio makubwa kwenye muziki wake msanii huyo alivunja mkataba wao na kutumikia nchini Canada ambako anaishi kwa sasa.

Read More
 Ykee Benda amkingia kifua Gravity Omutujju kwa kuwavunjia heshima wasanii wakongwe.

Ykee Benda amkingia kifua Gravity Omutujju kwa kuwavunjia heshima wasanii wakongwe.

Bosi wa lebo ya mpaka Records, Ykee Benda amemkingia kifua rapa Gravity Omutujju kutokana na kauli yenye utata aliyotoa juzi kati dhidi ya wasanii Bobi Wine, Bebe Cool na Jose Chameleone. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Ykee amesema hatua ya Omotujju kuwataka wasanii hao kustaafu muziki na kuwaapisha wasanii wajanga ilikuwa njia ya rapa huyo kutengeneza mazingira ya kuzungumzia mtandaoni. Ykee Benda amesema kauli ya hitmaker huyo wa “Enyama” haikulenga kumvunjia heshima msanii yeyote bali alitoa matamashi hayo kwa ajili ya kuteka hisia za mashabiki kabla kuachia wimbo wake mpya. Hata hivyo amewalaumu wasanii wakongwe kwa kuwaaminisha wasanii wajanga kuwa hawezi toboa kisanaa bila kujihusisha na matukio yenye ukakasi. Utakumbuka baada ya Gravity Omutujju kuwataka wasanii Bobi Wine, Bebe Cool na Jose Chameleone alikashifiwa na baadhi ya wasanii pamoja na mashabiki jambo ambalo lilimlazimu kuomba radhi kwa kuwavunjia heshima wasanii hao mbele ya waandishi wa habari.

Read More
 YKEE BENDA AGEUKIA BIASHARA YA KUANDAA MATAMASHA YA MUZIKI

YKEE BENDA AGEUKIA BIASHARA YA KUANDAA MATAMASHA YA MUZIKI

Staa wa muziki kutoka Uganda Ykee Benda ametangaza kujikita zaidi katika shughuli ya kuandaa maonesho ya muziki. Katika mahojiano yake hivi karibuni Ykee Benda amesema wameamua kuwekeza pesa zao kwenye matamasha ya muziki kwani wasanii wanaposainiwa kwenye lebo za muziki wanaleta hasara badala ya faida, kitendo ambacho kimemkatisha tamaa kwenye masuala ya kulea vipaji. Hitmaker huyo wa “My Babe” amesema lebo yake ya Mpaka Records haitomsaini msanii yeyote katika siku za hivi karibuni  hadi pale atakapoweka mambo sawa kwa upande wake. Utakumbuka baada ya msanii Dre Cali kujiondoa kwenye lebo ya Mpaka Records bila kufuata taratibu zinazofaa aliacha lebo hiyo ikakadiria hasara ya maelfu ya pesa kitu ambacho kimemfanya bosi wa lebo hiyo kuja na mbinu mpya kujiboresha kiuchumi.

Read More
 YKEE BENDA AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA

YKEE BENDA AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA

Mwanamuziki kutoka Uganda Ykee Benda amemtambulisha msanii wake mpya chini lebo yake ya muziki ya Mpaka Records. Msanii huyo aitwaye Chembazz atakuwa chini ya mpaka records ambayo itasimamia kazi zake za muziki na tayari ameachia ngoma yake mpya iitwayo “Ntufeelinga” akiwa amemshirikisha bosi wake Ykee Benda. Chembazz anachukua nafasi ya Dre Cali ambaye alitimukia nchini Canada baada ya kuingia kwenye ugomvi na Ykee Benda kutokana na kesi iliyokuwa ikimuandama ya uongozi wake wa zamani wa Wyse Technologies.

Read More
 YKEE BENDA APINGA UCHAGUZI WA UMA KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO

YKEE BENDA APINGA UCHAGUZI WA UMA KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO

Mwanamuziki kutoka Uganda Ykee Benda amepinga hatua ya Chama cha Wanamuziki nchini humo UMA kutaka kufanya uchaguzi kwa njia ya mtandao. Katika mahojiano yake hivi karibuni Ykee Benda amesema upigaji kura ukifanyika mtandaoni hatokuwa na uwazi kwa sababu matokeo yanaweza kubadilishwa na watu wanaosimamia maswala ya mitandao. Msanii huyo ambaye alikuwa rais wa zamani chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA amependekeza uchaguzi wa chama hicho kuandaliwa kwa mfumo wa kawaida wa watu kupiga foleni kwenye vituo vya upigaji kura. Hata hivyo ameutaka uongozi wa UMA kuomba usaidizi wa kifedha kutoka kwa mashirika ya kijamii na serikali kufadhili maandalizi ya uchaguzi wa kuwateua viongozi wapya wa chama hicho kama kweli hawana pesa za kutosha za kuandaa uchaguzi huo.

Read More
 YKEE BENDA AFUNGUKA SABABU ZA KUTAKA KUWA MUISLAMU

YKEE BENDA AFUNGUKA SABABU ZA KUTAKA KUWA MUISLAMU

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Ykee Benda ameweka wazi matamanio yake ya kubadili dini kutoka ukristo kwenda Uislamu. Akiongea na waandishi wa habari nchini uganda, ykee benda amefichua kuwa anaipenda dini ya Kiislamu kutokana na mambo mazuri yanayoambatana nayo, ikiwa ni pamoja na kuoa wanawake wanne ambayo ni tofauti na dini nyingine. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Farmer” amesisitiza kuwa anapenda jinsi wake wenza wanavyoishi pamoja katika ndoa za Kiislamu bila ya kuwa na migogoro, jambo ambalo ni nadra katika dini nyingine. Ykee Benda ni baba wa mtoto mmoja na uhusiano wake wa kimapenzi unaripotiwa kuwa unasuasua na ndiyo sababu anafikiria kubadili dini kuwa Muislamu. Bosi huyo wa Mpaka Records amefunguka kuhusu nia yake ya kusilimu wakati akiwapa chakula Waislamu huko Kireka nchini uganda wakati wa sherehe za Eid.

Read More
 YKEE BENDA AVUNJA UKIMYA WAKE KUHUSU SAKATA LA MUZIKI WAKE DRE. CALI

YKEE BENDA AVUNJA UKIMYA WAKE KUHUSU SAKATA LA MUZIKI WAKE DRE. CALI

Staa wa muziki nchini Uganda Ykee Benda amevunja kimya chake kuhusu ishu ya kukosana vibaya na msanii wake Dre Cali kiasi cha kurushiana makonde walipoingia kwenye ugomvi mkali wa pesa. Katika barua aliyochapisha kwenye mtandao wa Twitter Ykee Benda amesema hana ugomvi wowote na Dre. Cali kama inavyoripotiwa mtandaoni huku akidai kuwa lebo ya muziki ya Mpaka Records bado ina ukaribu na msanii huyo na famili yake ambapo hivi karibu  watanyosha maelezo kuhusu safari ya msanii huyo nchini Canada. Ykee Benda kupitia barua hiyo amesema kama kutakuwepo na utofauti kati yao wawili itasuluhishwa kwa njia ya amani huku akiongeza kuwa maelezo zaidi yatawekwa wazi kwa umma hivi karibuni. Uvumi wa Ykee Benda kutokuwa na uhusiano mzuri msanii wake Dre Cali ulianza mara baada ya msanii huyo kutoonekana kwenye afisi za lebo ya muziki ya Mpaka Records kwa muda jambo ambalo lilimlazimu Ykee Benda kuvunja kimya chake.

Read More
 YKEE BENDA AWATAKA WASANII WA UGANDA KUTOKUBALI KUTUMIWA VIBAYA NA MAPROMOTA WA MUZIKI

YKEE BENDA AWATAKA WASANII WA UGANDA KUTOKUBALI KUTUMIWA VIBAYA NA MAPROMOTA WA MUZIKI

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Ykee Benda amewataka wasanii wenzake kuanza kuwalipisha pesa nyingi mapromota wa muziki nchini humo ambao wanawaleta wasanii wa Nigeria kwenye shows zao. Bosi huyo wa Mpaka Records amewataka wasanii wenzake kuwa na msamimo dhabiti dhidi ya mapromota hao ili waweze kuwalipa pesa sawa na wasanii wa Nigeria kwani wana uwezo wa kufanya hivyo. Kauli ya Ykee Benda inakuja siku chache baada ya kuwataka mapromota muziki nchini Uganda kuwazingatia wasanii wa ndani kwenye shows zao badala ya kuwapa kipau mbele za wasanii wa nje.

Read More
 YKEE BENDA AWAPA CHANGAMOTO MAPROMOTA WA MUZIKI KUWAPA WASANII WA NDANI KIPAU MBELE KWENYE SHOWS ZAO.

YKEE BENDA AWAPA CHANGAMOTO MAPROMOTA WA MUZIKI KUWAPA WASANII WA NDANI KIPAU MBELE KWENYE SHOWS ZAO.

Bosi wa lebo ya muziki ya Mpaka Records, Ykee Benda ametoa wito kwa mapromota wa muziki nchini uganda kutowapa wasanii wa nigeria kipau mbele kwenye shows zao. Ykee Benda amesema tangu Rais Yoweri Museveni afungua uchumi wa nchi ya Uganda mapromota wengi nchini humo wamekuwa na mazoea ya kuwapa nafasi wasanii wa Nigeria kwenye shows zao huku wasanii wa ndani wakisahaulika. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Obangaina” amesema mapromota wa muziki  hawawatendei haki wasanii wa Uganda kwa kuwanyima shows ikizingatiwa kuwa hawajatumbuiza kwa kipindi cha miaka miwili tangu ujio wa Corona. Hata hivyo mashabiki wengi wa muziki nchini Uganda wamewataka wawekeze kwenye kazi zao za muziki kwani wengi wamekuwa wakiachia nyimbo ambazo hazikithi vigezo vya kimataifa wakiwa na imani kuwa zitafanya vizuri sokoni. Katika kipindi cha wiki mbili iliyopita,wasanii wawili wa nigeria chike pamoja na Ruger wamefanya shows kali nchini uganda huku wasanii wengi kutoka nigeria wakitarajia kuzuru uganda kwa ajili ya shows zao hivi karibuni.

Read More
 YKEE BENDA AAPA KUTOFANYA KAZI TENA NA WASANII WA NIGERIA

YKEE BENDA AAPA KUTOFANYA KAZI TENA NA WASANII WA NIGERIA

Mwanamuziki kutoka nchini uganda Ykee Benda amefunguka changamoto za kufanya kazi na wasanii wanigeria. Katika mahojiano na Galaxy FM Ykee benda amehapa kutofanya kazi tena na wasanii wa nigeria na ikitokea amefanya nao ngoma ya pamoja itakuwa ni wao wamemtafuta Hitmaker huyo wa “Banange” amedai baadhi ya wasanii wa Nigeria hawana moyo wa kuwasaidia wasanii wa mataifa mengine ya Afrika kwani mara nyingi wamekuwa wakiwaachia wasanii wa uganda mzigo wa kutangaza kolabo ambazo wameshafanya nao jambo ambalo anadai sio sawa. Bosi huyo wa lebo ya muziki ya Mpaka Records ameenda mbali Zaidi na kusema kuwa wasanii wa wanigeria wanafaidi pakubwa na kolabo za wasanii wa Uganda ikizingatiwa kuwa kolabo hizo zinawasaidia kupenya kwenye soko la muziki Afrika mashariki. Utakumbuka kipindi cha nyuma ykee benda alifanya kazi ya pamoja na msanii wa nigeria Rikado Banks kupitia singo inayokwenda kwa jina la time table lakini singo hiyo haukupata promotion ya kutosha kutokana na rikado banks kudinda kuipromote licha ya kuwa ngoma kali

Read More
 YKEE BENDA ATAKA SERIKALI YA UGANDA KUTENGA SIKU YA KITAIFA KUMKUMBUKA MAREHEMU MOZEY RADIO

YKEE BENDA ATAKA SERIKALI YA UGANDA KUTENGA SIKU YA KITAIFA KUMKUMBUKA MAREHEMU MOZEY RADIO

Bosi wa lebo ya muziki ya Mpaka Records msanii Ykee Benda ameitaka serikali ya Uganda kuiweka Februari mosi ya kila mwaka kuwa Sikikuu ya Kitaifa kumkumbuka Marehemu Mozey Radio ambaye alifariki tarehe hiyo mwaka wa 2018. Akizungumza huko Kagga nchini Uganda ambako Mozey Radio alipumzishwa mwaka wa 2018, Ykee Benda amesema mwendazake mozey Radio alikuwa nguzo muhimu katika taifa la uganda, hivyo ni vigumu kujaza pengo aliloliacha kwenye tasnia ya muziki nchini humo. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Obangaina” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kipindi anachipukia kwenye tasnia ya muziki nchini uganda alikuwa na mazoea ya kuiba mashairi ya nyimbo za mozey Radio na kuyatumia kwenye nyimbo zake.

Read More