RIPOTI: “ONLY ONE KING” YAFIKISHA STREAMS ZAIDI YA MILIONI 175

RIPOTI: “ONLY ONE KING” YAFIKISHA STREAMS ZAIDI YA MILIONI 175

Mtayarishaji wa muziki wa Bongofleva Yogo Beats ambaye amehusika kwa kiasi kikubwa kutengeneza album ya mwanamuziki Ali Kiba “Only One King” ameweka wazi kuwa album hiyo imefikisha zaidi ya streams million 175 katika digital platforms zote za kuuza na kusikiliza kazi za muziki. Kupitia ukurasa wake wa Instagram yake Yogo ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa muziki  katika tuzo za Tanzania Music Awards , ameeleza kuwa album hiyo ina jumla ya streams million 36 katika mtandao wa Boomplay huku ikiwa na streams million 16 katika mtandao wa wa Audiomack. Ikumbukwe album hiyo ambayo ilitoka mwezi Oktoba mwaka jana ikiwa na jumla ya nyimbo 16 za moto, ni album ya tatu kwa alikiba, baada ya Cinderella (2007) na AliK4Real (2009).

Read More
 PRODYUZA WA BONGOFLEVA YOGO BEATS ATANGAZA KUACHA MUZIKI

PRODYUZA WA BONGOFLEVA YOGO BEATS ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Prodyuza wa muziki wa Bongofleva, Yogo Beats ametangaza kuacha muziki bila kueleza sababu hasa iliyomplekea kuchukua maamuzi hayo magumu. Kupitia Instagram Yogo ameandika; I quit the game, staki tena muziki. f******** this game. Mara baada ya ujumbe huo, Wasanii na Maprodyuza mbalimbali wamemsihii asifanye hivyo kwenye post aliyoichapisha kwenye mtandao wa instagram. Hata hivyo, mtayarishaji mwenzake Mandugu Digital ame-comment kwa kuandika ujumbe unaosemeka “Mkitaka asiache milipeni fedha zake”,  ujumbe ambao umetafsiriwa kuwa huenda ni madeni anayowadai wasanii ndio imepelekea kuchukua maamuzi ya kutaka kuacha muziki. Yogo anafahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kutayarisha midundo ya muziki wa bongo fleva ambapo mbali na kufanya kazi nyingi na AliKiba, amewahi pia kutayarisha midundo ya wakali kama The Mafik, Nedy Music, Nandy na wengine kibao

Read More