YOUNG LUNYA AFUNGUKA MAENDELEO YA ALBUM YAKE MPYA

YOUNG LUNYA AFUNGUKA MAENDELEO YA ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa Hip Hop Tanzania, Young Lunya amesema albamu yake imeshamilika kwa asilimia 90, na sasa vimebakia vitu vichache vya mwisho kama mixing, mastering na kupangiwa tarehe ya kutoka na Sony Music. Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Sony Music Africa Juni 3, 2022, tayari Lunya yupo kwenye maandalizi ya albamu yake ya kwanza ambayo amewashirikisha Diamond Platnumz, Khaligraph Jones, Sho Madjozi na wengineo. Lunya amesema kufanya kazi na wasanii kama Diamond Platnumz, Khaligraph Jones na Sho Madjozi katika albamu hiyo ni hatua nyingine ya ukuaji wa muziki wake kibiashara na kimataifa. “Ni hatua nzuri kufanya kazi na msanii kama Diamond kwa sababu unakuwa unafanya kazi na msanii ambaye anajua biashara ya muziki, anajua nini kinafanyika, anataka hiyo kazi ije kuwa fedha, kwa hiyo ni kitu kikubwa sana,” amesema. “Ukija Kenya, Khaligraph Jones ni msanii anayefanya sana vizuri huko, kufanya naye kazi itanisaidia sana mimi kupenya Kenya kirahisi. Sho Madjozi wa Afrika Kusini ni msanii mkubwa kule kwao, ngoma zake zimefanya vizuri duniani, kwa hiyo ni kitu kizuri kufanya nao kazi” amesema Lunya. Hadi sasa kwa Tanzania Young Lunya ameshafanya kolabo na wasanii kama Ommy Dimpoz, Nikki wa Pili, Mabantu, Country Boy, Maua Sama, Rosa Ree, Joh Makini, Mimi Mars, Haitham Kim, Moni Centrozone, Harmonize, Profesa Jay na wengineo

Read More
 YOUNG LUNYA ADAI KUSAINI NA SONY MUSIC ILIKUWA NDOTO YAKE YA MUDA MREFU

YOUNG LUNYA ADAI KUSAINI NA SONY MUSIC ILIKUWA NDOTO YAKE YA MUDA MREFU

Msanii wa Hip Hop Tanzania, Young Lunya amesema kusainiwa na Sony Music Africa ilikuwa ni kiu yake ya muda mrefu kwani lengo lake ni kufikisha muziki wake kimataifa na tayari alishajiandaa kwa hatua hiyo. Young Lunya amesema ngoma zake nyingi alizorekodi zinalenga soko la kimataifa, hivyo alikuwa anahitaji Menejimenti yenye uzoefu katika eneo hilo, hivyo kuwa chini ya Sony Music ni mafanikio kwake. “Nimeipokea kwa furaha kwa sababu ndoto zangu zilikuwa ni kuja kufanya kazi na lebo kubwa ndio maana hata kazi zangu ambazo nilikuwa nazirekodi nilikuwa sizitoi hadi nije kupata uongozi ambao unakuwa unaelewa sana masuala ya muziki, kwa hiyo kwenda Sony Music ni kitu kikubwa sana,” amesema Lunya. Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Sony Music Africa Juni 3, 2022, tayari Lunya yupo kwenye maandalizi ya albamu yake ya kwanza ambayo amewashirikisha Diamond Platnumz, Khaligraph Jones, Sho Madjozi na wengineo. Huu ni usajili ya pili uliyoufanya Seven Mosha tangu alipoteuliwa kuwa Msimamizi wa Masoko na Maendeleo ya Wasanii Afrika Mashariki chini ya Sony Music Entertainment, msanii wa kwanza kumsaini ni Ferregola toka DR Congo ambaye ameshaachia albamu yake, Dynastie yenye nyimbo 16. Wimbo wa kwanza kwa Young Lunya kuuachia chini ya Sony Music unaitwa ‘Vitu Vingi’ ambao amesema unazungumzia mahusiano ya kimapenzi. “Nimezungumzia kwamba kichwa kina vitu vingi ila haimaanishi kwamba sikupendi (mpenzi wake). Bado napambana kwa ajili yako, kwa hiyo ni wimbo wa kimapenzi lakini wa kitofauti kidogo”.

Read More
 SONY AFRICA YAWEKA WAZI KOLABO ZA YOUNG LUNYA ZITAKAZO TOKA KARIBUNI

SONY AFRICA YAWEKA WAZI KOLABO ZA YOUNG LUNYA ZITAKAZO TOKA KARIBUNI

Mara baada ya Rapa Young Lunya kutoka nchini Tanzania kusaini kuwa chini ya Sony Music Africa, lebo hiyo ya kimataifa imeweka wazi kolabo kubwa za Rapa huyo zinazotarajiwa kutoka siku za mbeleni. Katika taarifa yao kwa umma, Sony Music wamesema kuna ngoma za Lunya zinazokuja alizoshirikiana na Khaligraph Jones, Shomadjozi na Diamond Platnumz. Katika hatua nyingine, Sony Music wametangaza kuwa Juni 10, mwaka wa 2022 Young Lunya ataachia wimbo wake mpya, uitwao Vitu Vingi ambao utakuwa wa kwanza chini ya lebo hiyo. Utakumbuka Sony Music Africa imewahi kufanya kazi na wasanii wa Tanzania kama Rose Muhando, Alikiba na wengine wengi.

Read More
 YOUNG LUNYA ATHIBITISHA KUSAINIWA ROCKSTAR

YOUNG LUNYA ATHIBITISHA KUSAINIWA ROCKSTAR

Rapa kutoka nchini Tanzania Young Lunya amethibitisha kusaini kufanya kazi na lebo kubwa ya muziki Afrika Rock Star ambayo pia inafanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa za muziki duniani. Akieleza hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Young Lunya amesema mchongo huo ulikuja kupitia verse ya freestyle aliyoposti kwenye kurasa zake za mitandao ya Kijamii. Mkali huyo ambaye pia ni msanii bora wa Hip Hop wakiume kwa mwaka 2021 kupitia tuzo za Muziki Tanzania (TMA), lebo yake hii mpya ishawahi kufanya kazi na wasanii kama AliKiba, Baraka The Prince na Lady Jay Dee. Kauli yake imekuja wiki kadhaa zilizopita baada ya Lebo ya Rockstar Africa kutangaza rasmi kuwasaini wasanii kutoka nchini Tanzania ambao ni Abby Chams na Aslay. Rockstar Africa ni label inayofanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment na ilianzishwa mwaka 2015 na Mtanzania Christine β€˜Seven’ Mosha ambaye ndiye muanzilishi na mmiliki.

Read More