Young Thug Adokeza Kuacha Muziki, Atamani Kuwa Streamer

Young Thug Adokeza Kuacha Muziki, Atamani Kuwa Streamer

Msanii maarufu wa Hip Hop, Young Thug, ameibua gumzo baada ya kueleza dhamira ya kuachana na muziki na kuhamia kwenye ulimwengu wa ustreaming. Akiwa mubashara na streamers maarufu Adin Ross na Neon, alieleza kuwa amechoka na muziki na anatamani kujikita katika maisha ya utangazaji wa moja kwa moja. Kauli hiyo imeibua mijadala mitandaoni, wengi wakihusisha hatua hiyo na kuvutiwa kwake na maisha ya streamers, ambayo alielezea kuwa ni huru, ya kusafiri mara kwa mara na yenye mapato makubwa kwa muda mfupi. Pamoja na hayo, hakuna taarifa rasmi kutoka kwa menejimenti yake, na baadhi ya wachambuzi wanaamini huenda kauli hiyo ni sehemu ya mbinu za kutangaza albamu yake mpya “UY Scuti”, inayotarajiwa kutoka mwezi huu wa Juni. Young Thug, ambaye amekuwa mmoja wa vinara wa muziki wa trap kwa zaidi ya muongo mmoja, bado anapewa nafasi na mashabiki kuendelea na kazi yake ya muziki licha ya dalili hizo za kutaka kubadili mwelekeo.

Read More
 ASAP Rocky Azima Tetezi za Albamu ya Pamoja na Young Thug

ASAP Rocky Azima Tetezi za Albamu ya Pamoja na Young Thug

Rapa maarufu kutoka Marekani, ASAP Rocky, amevunja kimya na kuzima uvumi uliokuwa ukisambaa mitandaoni kuhusu uwezekano wa kutoa albamu ya pamoja na Young Thug. Tetezi hizo zilianza kushika kasi jana baada ya ASAP Illz, mmoja wa wanachama wa ASAP Mob, kuashiria uwezekano wa collabo hiyo kupitia ujumbe wa kuvutia kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo, ASAP Rocky amekatisha matumaini ya mashabiki kupitia mtandao wa X kwa kuweka wazi kuwa hilo halipo kwenye mipango kwa sasa “FALESE MY BROTHER, UY SCUTI OTW” kwa tafsiri ya haraka: “Umesema uongo kaka, UY Scuti iko njiani”. Aliandika Kauli hiyo inaonyesha kuwa badala ya albamu ya pamoja, ASAP Rocky anajiandaa kuachia mradi wake binafsi unaoitwa UY Scuti, ambao tayari umeanza kuvutia hisia miongoni mwa mashabiki wake. Ingawa collabo kati ya Rocky na Thug bado ni ndoto kwa sasa, mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu kufahamu zaidi kuhusu UY Scuti, huku wakifuatilia kila dalili kutoka kwa rapa huyo anayejulikana kwa ubunifu na mitindo isiyotabirika.

Read More
 Young Thug Amshambulia Kid Cudi kwa Madai ya Kutoa Ushahidi Dhidi ya Diddy

Young Thug Amshambulia Kid Cudi kwa Madai ya Kutoa Ushahidi Dhidi ya Diddy

Mastaa wawili wa muziki wa hip hop, Young Thug na Kid Cudi, wameingia kwenye mzozo wa wazi baada ya Cudi kuonekana mahakamani kutoa ushahidi unaomkabili rapa nguli Sean “Diddy” Combs, katika kesi inayohusisha tuhuma za unyanyasaji, ukatili na matumizi mabaya ya madaraka. Kupitia chapisho aliloliweka kwenye akaunti yake ya X (zamani Twitter), Young Thug aliandika neno “rat” huku akimtag Kid Cudi, kauli ambayo katika muktadha wa mitaani na muziki wa hip hop humaanisha msaliti au mtu anayewasaliti wenzake kwa kushirikiana na vyombo vya sheria. Ingawa Thug alifuta chapisho hilo muda mfupi baadaye, tayari liliwasha moto mitandaoni, huku mashabiki wakitofautiana kuhusu uhalali wa hatua hiyo. Kid Cudi alionekana kizimbani mwishoni wiki jana kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili Diddy, msanii na mfanyabiashara mwenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya muziki wa Marekani. Taarifa zinasema ushahidi wa Cudi unahusiana na matukio ya zamani ambayo huenda yakawa na uzito mkubwa katika uamuzi wa mwisho wa kesi hiyo. Young Thug, ambaye kwa sasa naye anakabiliwa na kesi kubwa ya RICO (Racketeer Influenced and Corrupt Organizations Act) inayohusisha mashitaka ya uhalifu wa genge, ameonekana kuchukulia hatua ya Cudi kama ukiukaji wa kanuni za mtaa, zinazokataza kushirikiana na mamlaka au kutoa ushahidi dhidi ya wenzako. Wachambuzi wa masuala ya burudani wanasema huenda Thug anaangalia hali hiyo kwa jicho la mtu anayepitia mchakato wa kisheria na kuona kwamba hatua kama ya Cudi zinaweza kudhuru watu walioko kwenye mazingira kama yake. Kauli ya Thug imezua mijadala mikubwa, huku upande mmoja wa mashabiki ukimtetea Kid Cudi kwa kusema kwamba hatua yake ni ya kijasiri na inalenga kusaidia kutendeka kwa haki. Wengine wanasema Cudi amevunja misingi ya mshikamano katika jamii ya hip hop kwa “kuwageuka” wenzake. Mpaka sasa, Kid Cudi hajajibu moja kwa moja tuhuma au kejeli hizo kutoka kwa Young Thug. Vyanzo vya karibu na msanii huyo vinaeleza kuwa ameweka mkazo kwenye ukweli na kutafuta haki kwa waathirika.

Read More
 Kaka wa Young Thug akiri kosa mahakamani

Kaka wa Young Thug akiri kosa mahakamani

Kaka wa rapa Young Thug aitwaye Quantavious Grier “Unfoonk” amekiri makosa yake mahakamani na kuingia makubaliano maalumu kwamba asiwe na mawasiliano na Young Thug. Kwa mujibu wa Wbstv rekodi za mahakama ya jimbo la fulton zinaonyesha kuwa Quantavious Grier alikiri shtaka moja la kukiuka sheria inayopambana na rushwa (rico) na shtaka moja la wizi kwa kupokea mali ya wizi. Unfoonk, alikubali kifungo cha miaka 12 huku miaka miwili ikibadilishwa kuwa muda uliotumika na miaka 10 ni kifungo cha nje chini ya uangalizi Hata hivyo kuna masharti ambayo Grier atalazimika kuyatimiza kama sehemu ya kifungo chake cha nje. Masharti hayo ni pamoja na asifanye mawasiliano yoyote na kaka yake Young Thug pamoja na washtakiwa wengine hadi kesi hiyo imalizike. Lakini pia katika saa 750 afanye shughuli za kijamii lakini kutotoka nje na kutomiliki bunduki.

Read More
 YOUNG THUG AFUNGULIWA MASHTAKA NA PROMOTA

YOUNG THUG AFUNGULIWA MASHTAKA NA PROMOTA

Rapa kutoka Marekani Young Thug yupo korokoroni tangu mwezi Mei mwaka huu, hii imepelekea kuharibu baadhi ya mipango yake mingi ikiwemo kutofanyika kwa maonesho ambayo tayari alikuwa ametakiwa kuyafanya. Kwa mujibu wa The Atlanta Journal Constitution, Thug amefunguliwa mashtaka na promota wa kampuni ya A-1 Concert Entertainment kwa kutofanya onesho ambalo alitakiwa kufanya mwezi June mwaka huu. Waandaaji hao wanataka alipe pesa yao ya utangulizi kiasi cha shilling million 17.9 za Kenya. Ripoti zinasema, Thug alitafutwa mwezi January kwa ajili ya makubaliano ya kufanya show hiyo ya dakika 45 kwa malipo ya shilling million 35.9 lakini kuwa kwake Jela hadi leo kumemfanya kutotimiza makubaliano ya kutumbuiza.

Read More
 RAPPER YOUNG THUG KUTOKA MAREKANI KUSAIDIA WAAFRIKA UKRAINE

RAPPER YOUNG THUG KUTOKA MAREKANI KUSAIDIA WAAFRIKA UKRAINE

Rapa Kutoka  Nchini Marekani Young Thug ameonesha kuwa na moyo wa uhuruma baada ya kuguswa na kitendo cha Watu weusi nchini Ukraine kuachwa vitani huku wazungu wakisafirishwa sehemu salama zaidi. Kitendo hicho cha kibaguzi kimemgusa Rapa Young Thug ambaye amejitokeza na kusema kuwa yupo tayari kutoa msaadakwa Waafrika waliokwama kuondoka Ukraine kipindi hichi cha vita na Urusi. Hata hivyo amewaomba marapa wengine kushirikiana kufanikisha hilo huku akizitaka familia za waafrika waliokwama nchini Ukraine kumcheki kwa kuwa taratibu za kuondoka nchini humo kwa sasa ni ngumu.

Read More