YY Amtema Mpenzi Baada ya Kukosa Kutandika Kitanda

YY Amtema Mpenzi Baada ya Kukosa Kutandika Kitanda

Mchekeshaji maarufu wa Kenya, YY Comedian, amefichua kisa cha kushangaza kuhusu maisha yake ya mapenzi ya zamani. Akizungumza katika kipindi cha Feast with Friends kinachoendeshwa na Shiksha Arora, YY alieleza kuwa aliwahi kumtema mwanamke mara baada ya mkutano wao wa kwanza kwa sababu alishindwa kutandika kitanda. Kwa mujibu wa msanii huyo, tukio hilo lilimfanya atathmini mitazamo na maadili ya mpenzi wake, jambo lililomsukuma kufikia uamuzi wa haraka wa kumaliza uhusiano. YY alisema kwake nidhamu na mpangilio ni mambo ya msingi katika maisha ya kila siku, na kushindwa kwa mwanamke huyo kutandika kitanda kulionekana kama ishara ya kutopenda usafi na kutojali mambo madogo. Kisa hicho kimezua mijadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakiona sababu hiyo kuwa ndogo mno kupelekea kuvunja uhusiano, huku wengine wakimtetea wakisema kila mtu ana haki ya kuweka viwango vyake vya maisha binafsi. YY Comedian amejulikana kwa ucheshi wake wa kipekee na mara nyingi hutumia matukio ya maisha binafsi kama chanzo cha vichekesho, jambo linalomfanya kuendelea kuwa miongoni mwa wakali wa tasnia ya ucheshi nchini Kenya.

Read More
 Mashabiki Wamtaja Rigathi kwenye Kauli ya YY Comedian Kuhusu Kipigo cha Harambee Stars

Mashabiki Wamtaja Rigathi kwenye Kauli ya YY Comedian Kuhusu Kipigo cha Harambee Stars

Mchekeshaji YY Comedian ameonyesha masikitiko yake kufuatia timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, kuondolewa na Madagascar katika robo fainali ya michuano ya CHAN 2024. YY, kupitia ukurasa wake wa Instagram, amedai huenda kulikuwa na bahati mbaya iliyosafirishwa kutoka nje ya nchi na mtu fulani, akitilia shaka matokeo hayo kwa kuzingatia rekodi nzuri ya Kenya kwenye michezo ya awali. Kauli hiyo imezua mjadala mitandaoni baada ya mashabiki kuhusisha dondoo za mchekeshaji huyo na kurejea kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kutoka Marekani siku moja kabla ya mechi, ambapo alihudhuria pambano hilo pamoja na mashabiki wengine wa Kenya. Kenya ilipoteza kwa mikwaju ya penalti 4-3, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida, matokeo yaliyokatisha matumaini ya mashabiki waliokuwa na imani kubwa kwa Harambee Stars kufika hatua za juu zaidi.

Read More
 Mchekeshaji YY Aomba Msamaha Kwa Kutania Pesa Ambazo Kenrazy Anatoza Kwenye Show

Mchekeshaji YY Aomba Msamaha Kwa Kutania Pesa Ambazo Kenrazy Anatoza Kwenye Show

Mchekeshaji wa YY ameomba msamaha kwa kutania kiasi cha pesa ambacho mwanamuziki wa Kenya Kenrazy anatoza kwenye shows zake. Katika mahojiano na Plug TV, YY alinukuliwa akisema kuwa hawezimudu gharama za kumualika msanii Willy Paul kwenye shows zake kwa kuwa anatoza pesa nyingi ambapo alienda mbali Zaidi na kutania kuwa ni heri ampe show timmy tdat pamoja na kenrazy kwa sababu wasanii hao hawahitaji pesa nyingi kutumbuiza kwenye shows. “Kama tusipokuafford, tutaita Timmy Tdat na atakuja Hadi na Kenrazy na 40k.” Alisema. Kauli hiyo ilionekena kumkera kenrazy ambaye alitumia ukurasa wake wa instagram kusema kwamba yy alimvunjia heshima kwa kuidharau na kuishusha brand yake ya muziki ambayo ametengeneza kwa muda na pia ni brand ambayo imekuwa ikimuingiza kipato ambacho kimemsaidia kukithi mahitaji ya familia yake. “Nimekuwa nikijitahidi sana kutengeneza chapa yangu kila siku na hivyo siwezi kubali kauli kama hiyo inayotoka kwa mtu kama wewe. Kwa kweli  umenikosea sana, nilidhani unanijua vizuri zaidi. Unaniona nafanya kazi kila siku bila faida yeyote kutoka kwenye tasnia hii na kulea familia yangu kwa miaka hiyo yote, hivyo kukejeli sana yangu ni jambo lisilokubalika.”, Kenrazy aliandika kwa masikitiko. Hata hivyo Comedian YY alilazimika kumuomba radhi msanii kenrazy kwa kusema kwamba anasikitika kumtania Kenrazy na kumfanya ajisikie vibaya, kwani hakuwa na nia ya kujeli brand au chapa yake ikizingatiwa kuwa ni msanii mkubwa ambaye ameacha alama kwenye muziki wa Kenya.

Read More