Zari Amshauri Mumewe Shakib Aachane na Masumbwi Baada ya Kipigo

Zari Amshauri Mumewe Shakib Aachane na Masumbwi Baada ya Kipigo

Socialite maarufu wa Uganda, Zari Hassan, ameripotiwa kumshauri mumewe Shakib Cham kuachana na mchezo wa masumbwi na kuelekeza nguvu zake katika shughuli nyingine za kibinafsi zinazoweza kumuingizia kipato. Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na wawili hao, Zari amekuwa mstari wa mbele kushauri mumewe kutokana na hali iliyoonekana baada ya pambano la hivi karibuni lililomshirikisha Shakib na msanii Rickman Manrick. Katika pambano hilo, Shakib alipokea makonde mazito ya kichwa yaliyopelekea kuanguka chini na kupoteza fahamu, hali iliyomlazimu muamuzi kusitisha pambano hilo mara moja. Tukio hilo lilimuumiza mno Zari ambaye alishuhudia mumewe akizirai ulingoni na kulia machozi ya uchungu. Chanzo hicho kimeeleza kuwa, licha ya juhudi za Shakib kujaribu kujiweka kwenye tasnia ya masumbwi ya burudani, mchezo huo haujaweza kuleta mapato yaliyotarajiwa na badala yake umekuwa chanzo cha hofu na maumivu kwa familia.

Read More
 Zari Hassan Aangua Kilio Baada ya Shakib Kupigwa Knockout na Rickman

Zari Hassan Aangua Kilio Baada ya Shakib Kupigwa Knockout na Rickman

Mfanyibiashara na sosholaiti maarufu, Zari Hassan, alijikuta akibubujikwa na machozi baada ya mumewe, Shakib Cham, kupigwa knockout vibaya na msanii Rickman Manrick katika pambano la masupastaa lililoshuhudiwa usiku wa Jumamosi, 30 Agosti 2025, ndani ya MTN Arena, Lugogo. Pambano hilo lililokuwa limevuta maelfu ya mashabiki lilimalizika mapema katika raundi ya pili, baada ya Rickman kumshushia Shakib ngumi nzito pande zote za kichwa na kumwangusha chini akipoteza fahamu. Umati ulilipuka kwa shangwe, lakini macho yote yalihamia moja kwa moja kwa Zari, aliyekuwa safu ya mbele, akishuhudia mume wake akizimwa ringini. Awali, Zari alionekana akishangilia kwa nguvu akimhimizia mumewe kupambana, lakini alibadilika ghafla na kuangua kilio mara tu Shakib alipoanguka chini bila msaada. Alimkimbilia ulingoni, akimshika na kumfariji huku akibubujikwa na machozi, jambo lililoacha taswira ya aibu mbele ya umati na kamera zilizokuwa zikirekodi kila tukio. Mitandaoni, mashabiki hawakuchelewa kumrushia vijembe, wakimuita “First Lady wa Knockout”, huku wengine wakisema “hata machozi ya Zari hayawezi kufuta aibu ya kipigo cha Shakib.” Wengine walimkejeli kuwa safari hii si biashara zake wala mitindo yake ya kifahari iliyokuwa gumzo, bali machozi yake ringini. Rickman kwa upande wake aliendeleza rekodi yake ya ushindi, akipata ushindi wa pili katika michezo ya masupastaa baada ya kumbwaga pia msanii Grenade Official mnamo Desemba 2024. Kwa Shakib na Zari, pambano hili limeacha kumbukumbu chungu, knockout kwa ulingo, na machozi kwa jukwaa la mbele.

Read More
 Zari Hassan akatisha mkataba na hoteli moja nchini Uganda kwa kuvujisha picha zake za faraghani

Zari Hassan akatisha mkataba na hoteli moja nchini Uganda kwa kuvujisha picha zake za faraghani

Soshalaiti’ na mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Zari Hassan amekatisha mkataba wake na hoteli moja ya kifahari nchini Uganda ambapo alikuwa mapumzikoni na mpenzi wake Shakib Cham. Zari ametangaza kuvunja mkataba wake na Divine Resort & Spa baada ya mpiga picha mmoja wa hoteli hiyo kukiuka kifungu cha mkataba wao kilichosema kwamba picha na video zote zinapaswa kuidhinishwa na Zari kabla ya kuachiwa. “Mpiga picha huyo ameweka picha za Zari kabla ya kuidhinishwa. Kuanzia sasa, Zari hatabanwa tena na mkataba huo na hata-tag Divine Resort AndS pa kwenye chapisho zake zozote za mitandao ya kijamii,” sehemu ya barua ya kusitishwa kwa Mkataba huo imeeleza. Katika barua hiyo, Zari ambaye ni zamani wa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz alitoa agizo kwa mpiga picha mhusika kufuta picha zake zote alizochapisha kwenye kurasa zake na zile ambazo alituma kwa wanablogu. Pia, aliizuia hoteli hiyo dhidi ya kutumia picha zake na mpenzi wake kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii au tovuti yao. “Kukosa kuzingatia yaliyo hapo juu kutahitaji timu kuendelea na hatua za kisheria na fidia,” barua hiyo ilieleza. Katika video aliyopakia kwenye Snapchat na Insta Story yake, Zari alidai kuwa mpiga picha huyo alivujisha picha hizo kwa sababu alitaka kuwa wa kwanza kutangaza habari za likizo yake na mpenzi wake kwenye blogu yake. Alilalamikia hatua hiyo na kusema kuwa mhusika alikosa weledi katika kazi yake na kukiuka makubaliano kati yake na hoteli. “Baadhi ya picha hizo ni nzuri na zingine kidogo ni PG 13,” alisema Zari.

Read More