Zari anyosha maelezo ishu ya kushindana na Zuchu kumteka kimapenzi Diamond Platnumz. 

Zari anyosha maelezo ishu ya kushindana na Zuchu kumteka kimapenzi Diamond Platnumz. 

Mrembo maarufu wa Uganda, Zari The Bosslady ameonyesha kuchukizwa na habari za uongo kuhusu kile kinachodaiwa yupo katika mashindano na Zuchu ili kuunasa moyo wa Diamond Platnumz. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari amesema “Halafu wajinga wote hapa wanaamini maoni hayo yaliyoambatanishwa na picha yangu? Nimekuwa nikiwaonya kuwa siku moja nitawashtaki kiwango cha nyinyi kuuza figo zenu ili mueze kunilipa. Wacheni uongo na upuzi. Shenzi type,” Kauli yake imekuja mara baada ya ukurasa mmoja wa Instagram kuweka picha iliyoonyesha Insta story za Zari akimsihi Zuchu kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz. Kwenye picha hiyo ‘Zari’ alisema kuwa Diamond ataishi kuwa mpenzi wake na mapenzi yake na Zuchu hayatadumu. Kwa sasa Zari The Bosslady ambaye amekuwa anaishi Afrika Kusini na familia yake, alijaliwa watoto wawili na Diamond Platnumz, Tiffah na Nillan.

Read More
 ZARI THE BOSSLADY ATOA ANGALIZO KWA MASHABIKI ZAKE MTANDAONI

ZARI THE BOSSLADY ATOA ANGALIZO KWA MASHABIKI ZAKE MTANDAONI

Mrembo Zari The Bosslady amezidi kuandamwa na page fake kwenye mitandao ya kijamii zinatumia jina lake na kuwalaghai watu wanatoa misaada kumbe lengo ni kuwaibia. Zari alishawahi kushtakiwa kutokana na utapeli uliofanyika kupitia page fake ya Facebook iliyotumia jina lake, hivyo kuwataka kushabiki wake kuwa makini. Kwa sasa amewaomba mashabiki wake ku-report channel ya YouTube inayotumia jina lake kwani tayari amefikishiwaa malalamiko kuhusu utapeli unaofanywa kupitia channel hiyo. Zari kutokea Uganda anayeishi Afrika Kusini na watoto wake watano, ni miongoni mwa wanawawe wenye nguvu kubwa ushawishi kwenye mitandao, hivyo baadhi ya watu kutumia hiyo kama fursa kujifunuisha kinyume cha sheria.

Read More