Ziza Bafana Alaumu Promoters Na Viongozi Kwa Kukwamisha Muziki Wa Uganda

Ziza Bafana Alaumu Promoters Na Viongozi Kwa Kukwamisha Muziki Wa Uganda

Msanii maarufu wa Dancehall nchini Uganda, Ziza Bafana, ameibuka na lawama kali dhidi ya waandaaji wa matamasha (promoters) na viongozi wa serikali, akiwalaumu kwa kuchelewesha maendeleo ya muziki wa Uganda na kuzuia wasanii wa taifa hilo kuvuka mipaka kimuziki. Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini humo, Bafana alisema kuwa promoters wengi nchini Uganda wamekuwa wakipendelea kufanya kazi na wasanii wasio na mpangilio wala chapa rasmi ya kisanaa. Kwa mujibu wa Bafana, hali hiyo imekuwa ikizuia maendeleo ya wasanii waliowekeza kikamilifu katika ubunifu, utaratibu na ujenzi wa chapa zao. “Waandaaji wa matamasha hawawaheshimu wasanii. Wanataka tu kufanya kazi na wale wasio na mpangilio wowote. Wakiona msanii aliye na chapa nzuri na amejiweka vyema, wanampiga vita hadi aanguke,” alisema kwa hisia. Kauli hiyo imeungwa mkono na mashabiki na wadau wa tasnia ya muziki ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia mazingira magumu ambayo wasanii wa Uganda hukabiliana nayo licha ya uwekezaji mkubwa katika utayarishaji na utangazaji wa kazi zao. Aidha, Ziza Bafana hakuishia kwa promoters pekee. Alielekeza lawama pia kwa viongozi wa serikali ya Uganda kwa kile alichokitaja kama ukosefu wa heshima na kuthamini sanaa.  “Viongozi wetu hawaheshimu sanaa. Hawaoni uzuri wake. Itahitaji mabadiliko makubwa ili sanaa iheshimiwe, na hapo ndipo tutaanza kuona maendeleo,” aliongeza. Kauli ya Ziza Bafana inakuja wakati ambapo mjadala kuhusu hadhi ya wasanii na mchango wa sekta ya burudani katika uchumi na utambulisho wa taifa unazidi kushika kasi, huku wasanii wengi wakihamasisha mageuzi katika mfumo wa usimamizi wa sanaa nchini Uganda. Mashabiki wamekuwa wakisubiri kuona kama kauli za Bafana zitachochea mjadala mpana zaidi unaoweza kuleta mabadiliko chanya kwa tasnia ya muziki nchini humo.

Read More
 Ziza Bafana Akanusha Taarifa za Ugomvi na Kalifah Aganaga

Ziza Bafana Akanusha Taarifa za Ugomvi na Kalifah Aganaga

Msanii wa muziki wa dancehall kutoka Uganda, Ziza Bafana, amefunguka kuhusu uhusiano wake na mwanamuziki mwenzake Kalifah Aganaga, akisema kwamba amekuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Aganaga katika tasnia ya muziki. Akizungumza katika mahojiano na Sanyuka Television, Ziza Bafana alikanusha madai kuwa alimshambulia Kalifah kwa maneno au kumdharau, akieleza kuwa alieleweka vibaya. Alisisitiza kuwa hana chuki yoyote dhidi ya Aganaga na hata hawezi kumkosea heshima. “Nilieleweka vibaya kwa sababu mimi binafsi sina ubaya wowote na Kalifah Aganaga. Sina nia mbaya kabisa. Kalifah ni kama ndugu yangu, na mimi ni mmoja wa watu waliomsaidia katika kujenga kazi yake ya muziki. Siwezi kumdharau,” alisema Bafana. Ziza Bafana na Kalifah Aganaga wote ni wasanii wakongwe kwenye muziki wa Uganda na wamewahi kushirikiana kwenye majukwaa mbalimbali. Kauli ya Bafana imekuja wakati ambapo mashabiki wamekuwa wakizungumzia uwezekano wa mgogoro kati yao, hali ambayo sasa inaonekana kufutwa na maelezo hayo ya amani. Mashabiki wamepokea taarifa hiyo kwa hisia tofauti, baadhi wakimtaka Bafana na Aganaga kurejea studio pamoja kama zamani, huku wengine wakisisitiza umuhimu wa umoja miongoni mwa wasanii wa Uganda.

Read More
 Nina Roz Akanusha Tetesi za Kutoka Kimapenzi na Ziza Bafana

Nina Roz Akanusha Tetesi za Kutoka Kimapenzi na Ziza Bafana

Msanii maarufu wa muziki wa Afrobeat, Nina Roz, amejitokeza wazi na kukanusha vikali uvumi unaosambaa mitandaoni kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na rapa Ziza Bafana. Katika mahojiano maalum na vyombo vya habari, Nina Roz alisema kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na Bafana, akisisitiza kwamba wao ni marafiki wa kawaida tu na hakuna chochote kinachoendelea kati yao. “Sijawahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na Ziza Bafana. Ni rafiki yangu wa kawaida tu, na tunaheshimiana kama wasanii,” alisema Nina Roz kwa msisitizo. Tetesi hizo zimekuwa zikienea mitandaoni, zikidai kuwa wawili hao wamekuwa wakionekana mara kwa mara pamoja, hali iliyoibua maswali miongoni mwa mashabiki. Hata hivyo, Nina ameweka wazi kuwa kukutana kwao kunatokana na ushirikiano wa kazi na si mapenzi. Msanii huyo pia alitumia fursa hiyo kuwakumbusha mashabiki wake kuhusu uhusiano wake wa awali na msanii mwenzake Daddy Andre, ambaye kwa sasa hawako pamoja. Nina alifafanua kuwa tangu alipoachana na Daddy Andre, hajahusika tena na uhusiano wa kimapenzi wa hadharani.  “Sijui lolote kuhusu hizo taarifa za mimi kutoka na Ziza Bafana. Sina muda wa kupoteza kwenye tetesi za mitandaoni,” aliongeza. Kwa sasa, Nina Roz anasema ameweka mkazo kwenye kazi yake ya muziki, akiandaa miradi mipya itakayozinduliwa hivi karibuni.

Read More
 Ziza Bafana akanusha madai ya kujiunga na siasa

Ziza Bafana akanusha madai ya kujiunga na siasa

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Ziza Bafana amepuzilia mbali madai ya kuacha muziki na kugeukia siasa. Kwenye mahojiano yake karibuni amekanusha kuwahi kuweka wazi na mpango wa kujiunga na siasa,ishara kwamba amejiondoa kwenye masuala mazima ya siasa nchini Uganda. Mnamo Juni 2022, Bafana alifichua jinsi alivyokuwa akifikiria sana kujiunga na siasa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2026 ambapo alienda mbali zaidi na kudokeza mpango wa kuwania ubunge mwaka 2026 kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi wa Masaka.

Read More
 Ziza Bafana awaasa wanawake kuwasaidia waume zao kiuchumi badala ya kuwa chombo cha starehe

Ziza Bafana awaasa wanawake kuwasaidia waume zao kiuchumi badala ya kuwa chombo cha starehe

Msanii wa Dancehall Ziza Bafana amewahimiza wanawake kutia bidii na kuwasaidia waume zao katika malezi ya familia. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Bafana ameeleza kuwa wanawake wengi hawawaungi mkono waume zao kifedha, jambo ambalo limepelekea baadhi ya wanaume kujiingiza kwenye madeni yanayowafilishisha kiuchumi. Hitmaker huyo wa “Akalulu” anaamini wanawake wanapaswa kutoa msaada zaidi katika mahusiano badala ya kujaribu kuwafurahisha wanaume kitandani kwani ngono ni jambo la ziada. “Wanawake wengi siku hizi wanapenda ngono, hafla za birthdays na baby showers. Mambo haya yamepelekea wanaume wengi kufilisika kiuchumi. Wanawake wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na kuwasaidia waume zao. Siwezi mvumilia mwanamke ambaye anatoa ngono tu katika mahusiano,” Ziza Bafana alielezea. Utakumbuka Ziza Bafana kwa sasa hana mpenzi anayejulikana kwa kuwa bado anamtafuta mwanamke wa ndoto yake.

Read More
 ZIZA BAFANA APINGA AZMA YA CINDY KUWA RAIS WA MUUNGANO WA WASANII UGANDA

ZIZA BAFANA APINGA AZMA YA CINDY KUWA RAIS WA MUUNGANO WA WASANII UGANDA

Msanii wa Dancehall kutoka nchini Uganda Ziza Bafana amejiunga na orodha ndefu ya wasanii ambao hawataki Cindy Sanyu arejee afisini kama Rais wa Muungano wa Wanamuziki nchini humo (UMA) kwa muhula wa pili. Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini Uganda, Hitmaker huyo wa ngoma ya “Speed Controlle” amesema anamuunga mkono King Saha kuwa rais wa muungano huo kwa kuwa Cindy amefikia kiwango anachohitaji kuzingatia zaidi majukumu yake ya kifamilia. “Tumemuinua. Amefanya makubwa. Sasa mwache arudi nyumbani akalee watoto wake. Nampenda kama dada, lakini namuunga mkono King Saha,” amesema Ziza Bafana ameenda mbali zaidi na kusema kwamba UMA inahitaji kiongozi shujaa na jasiri kufanikisha malengo ya muungano huo tofauti na Cindy ambaye amekuwa akikatishwa tamaa na maneno ya watu mtandaoni. Utakumbuka Cindy Sanyu atachuana na King Saha pamoja na Maurice Kirya kwenye kinyanganyiro cha kugombea urais wa muungano wa wasanii nchini Uganda kwenye uchaguzi utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Read More
 ZIZA BAFANA AMSHUSHIA KIPIGO DEEJAY KUTOKANA NA UBOVU WA SAUTI KWENYE MOJA YA PERFORMANCE YAKE

ZIZA BAFANA AMSHUSHIA KIPIGO DEEJAY KUTOKANA NA UBOVU WA SAUTI KWENYE MOJA YA PERFORMANCE YAKE

Inaonekana misala haiishi kwa Ziza Bafana, baada ya msala wa kutupwa jela kwa kususia moja ya show yake wiki kadhaa zilizopita licha ya kulipwa pesa zote, Mwanamuziki huyo kutoka nchini Uganda ameingia tena kwenye headlines. Hii ni baada ya kumshushia kichapo cha mbwa Deejay mmoja kwenye moja ya performance yake wikiendi hii iliyopita. Ziza Bafana ambaye alikuwa ameshikisha performance yake na mzuka wa kutosha, alikasirishwa na kitendo cha deejay kucheza nyimbo zake zilizokuwa na sauti mbovu. Msanii huyo alilazimika kusitisha kutoa burudani kwa mashabiki zake hadi pale Waandaaji wa onesho hilo walipomleta deejay mwingine ambaye aliweka mambo sawa. Hata hivyo baada ya hali kutulia, Ziza Bafana alisikika akiwaelezea mashabiki zake kuwa madeejay wakati mwingine wanaudhi kiasi cha kuwafanya wasanii kutaka kuwapiga kutokana na ubovu wa sauti za mashine zao.

Read More
 ZIZA BAFANA AACHIWA HURU BAADA YA KUKAMATWA HUKO KABALE, NCHINI UGANDA

ZIZA BAFANA AACHIWA HURU BAADA YA KUKAMATWA HUKO KABALE, NCHINI UGANDA

Mwanamuziki wa Dancehall kutoka nchini Uganda Ziza Bafana ameachiliwa uhuru baada ya kukamatwa Februari 13 huko Kabale. Bafana alikamatwa baada ya performace yake huko kabale nchini uganda huku sababu kubwa ya kukamatwa kwake ikitajwa kuwa alidinda kutumbuiza kwenye moja ya show huko kabale licha ya kulipwa pesa zote kabla ya ujio wa janga la korona, jambo lilowakasirisha waandaji wa show hiyo wakamtupa jela. Inaelezwa kuwa bafana alitaka mapromota wa show hiyo wamuongezee pesa kabla kutumbuiza kutokana na show hiyo kuwa na idadi kubwa ya watu. Baada ya msanii huyo kususia kutumbuiza, mashabiki walikasirishwa na kitendo hicho ambapo walizua vurugu na kuaharibu vitu vya thamani katika ukumbi wa kabale jambo lilowaacha mapromota wakikadiria hasara kubwa. Hata hivyo inaripotiwa kuwa mapromota waliompelekea kukamatwa kwake walihamua aachiwe uhuru kwa masharti kwamba atatumbuiza kwenye show nyingine itakayoandaliwa na waandaji wa show hiyo.

Read More
 ZIZA BAFANA AMCHANA BEBE COOL KISA ORODHA YAKE YA WASANII WALIOFANYA VIZURI MWAKA 2021

ZIZA BAFANA AMCHANA BEBE COOL KISA ORODHA YAKE YA WASANII WALIOFANYA VIZURI MWAKA 2021

Mwanamuziki anayesuasua kimuziki nchini Uganda Ziza Bafana hana furaha kabisa baada ya kutoonekana kwenye orodha ya wasanii wa kila mwaka ambayo hutolewa na msanii mwenzake Bebe Cool. Bafana, ambaye alifanya vizuri mwaka wa 2021 kwa kuachia magoma makali anadai kuwa Bebe Cool alipoteza mweelekeo katika tasnia ya muziki nchini Uganda kwani siku hizi hajakuwa akiachia muziki mzuri kama kipindi cha nyuma. Hitmaker huyo wa “Embuzi” amesema Bebe Cool,anatumia orodha yake ya kila mwaka ya wasanii waliofanya vizuri kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari nchini Uganda. Ikumbukwe Bebe Cool hajawahi kuwa na uhusiano mzuri na mwanamuziki mwenzake Ziza Bafana baada ya msanii huyo kuanza kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya miaka kadhaa iliyopita.

Read More