
Mastaa kadhaa wakubwa duniani akiwemo Future, Michael Jackson, Adele, Tyla na wengine wamepata matatizo baada ya kuripotiwa kuwa kurasa zao za Instagram zimevamiwa (hacked).
Kila akaunti iliyodukuliwa iliposti picha ile ile inayomuonesha mtu anayefanana na Future akiwa ameshika sarafu ya “Free Bandz” huku wakimtaja Future na kuweka anwani ya sarafu ya kidijitali (crypto address).
Tukio hili limezua taharuki kwa mashabiki, huku wengi wakijiuliza iwapo ni kampeni ya kutangaza crypto au ni uvamizi wa kweli wa mitandao ya kijamii. Wataalamu wa usalama mtandaoni wanashauri mashabiki kupuuza taarifa hizo hadi wasanii wahusika watakapotoa kauli rasmi. Hata hivyo baada ya muda mfupi Posti hizo zimefutwa kwenye kurasa za Mastaa hao, jambo linaloashiria huenda kweli walidukuliwa.