
Msanii kutoka Kenya Tanasha Donna amechefukwa, ameamua kuichana Label yake kwa kile anachodai kwamba imeachia wimbo wake mpya bila ridhaa yake.
Kupitia mfululizo wa Instastory zake kwenye mtandao wa Instagram Tanasha ameshangazwa na kitendo cha Ziiki kuachia ngoma hiyo bila ya makubaliano yoyote kwa kigezo kuwa haikuwa imefikia ubora uliohitajika na uongozi wa lebo hiyo.
Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba amechoshwa manyanyaso ambayo ameyapitia chini Label hiyo kwa muda miaka mitatu sasa huku akitishia kuichukulia Ziiki hatua kali za kisheria ili dunia ione udhalimu wake.
Hata hivyo amemalizia kwa kusema iwapo lebo hiyo ingekubali wamaliza tofauti zao nyuma pazia hangeanika malalamiko yake kwenye mitandao ya kijamii lakini kutokana na ujeuri wao ameamua kuweka wazi ghadhabu zake.