Tanasha Donna Atoa Tahadhari kwa Wanaomsema Vibaya Naseeb Junior

Tanasha Donna Atoa Tahadhari kwa Wanaomsema Vibaya Naseeb Junior

Msanii Tanasha Donna ameonyesha msimamo mkali na upendo wake kwa mwanawe, Naseeb Junior, baada ya kutuma ujumbe mzito unaoashiria kuwa yuko tayari kumlinda kwa gharama yoyote. Kupitia Instastory yake, Tanasha ameeleza kuwa hawezi kuvumilia mtu yeyote atakayemtaja vibaya au kumdhuru mtoto wake, akisisitiza kuwa yeyote atakayemgusa kwa njia yoyote atakuwa amejipatia adui wa maisha. Mrembo huyo, amesema upendo wake kwa Naseeb Junior ni wa dhati na wa kudumu, na kwamba atahakikisha anakuwa salama dhidi ya mashambulizi ya maneno au vitendo vinavyoweza kumuathiri. Tanasha amekuwa miongoni mwa wasanii wanaoweka wazi mapenzi yao kwa watoto wao, na mara nyingi huzungumzia jinsi uhusiano na mwanawe umembadilisha na kumpa nguvu mpya maishani.

Read More
 Tanasha Donna awapa somo mashabiki juu ya usafi

Tanasha Donna awapa somo mashabiki juu ya usafi

Mwimbaji wa muziki kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna amesistiza usafi kwa wanaume na wanawake. Tanasha amesema kwa mtu yeyote haijalishi anapitia changamoto gani katika maisha, lakini ahakikisha unanukia vizuri popote uendapo. “Sijui ni mara ngapi tutalizungumzia hili lakini watu wangu, wanawake kwa wanaume, usafi ni kitu cha muhimu sana. Ni muhimu sana watu wangu kama hamkuwa mnajua,” Tanasha Donna alianza kushauri. “Hakikisha unanukia vizuri si tu kwa kujirembesha kwa marashi kwa nje, lakini usafi halali. Hakikisha unanawa mikono yako, usisahau kufanya utaratibu wa kukoga kati ya mara mbili na mara tatu kwa siku, piga mswaki, tumia kopo la msalani vizuri na pia osha kwa maji baada ya kumalzia kukata gogo. Nyoa nywele zote mwilini mwako, kaa nadhifu,” alisema Tanasha. Aliendelea kwa kusema “Natumai wengi wenu mmesikia nukuu kuwa usafi humweka mtu karibu na kumcha Mungu, ni ukweli watu wangu. Utagundua kuwa kukiwa na uchafu karibu nawe unapoteza dira ya akili lakini wakati kuna usafi unahisi mwenye utulivu na amani. Miili yetu ni hekalu takatifu la Mungu, tuilinde wote wake kwa wanaume,” Alisema. hata hivyo mwanamuziki huyo amesema yeye hawezi kubaliana na wale wanaosema ‘mwanaume ni jasho’ huku akisema kudumisha usafi ni kwa watu wote.

Read More
 Tanasha akasirishwa na hatua ya label yake kuachia wimbo bila makubaliano

Tanasha akasirishwa na hatua ya label yake kuachia wimbo bila makubaliano

Msanii kutoka Kenya Tanasha Donna amechefukwa, ameamua kuichana Label yake kwa kile anachodai kwamba imeachia wimbo wake mpya bila ridhaa yake. Kupitia mfululizo wa Instastory zake kwenye mtandao wa Instagram Tanasha ameshangazwa na kitendo cha Ziiki kuachia ngoma hiyo bila ya makubaliano yoyote kwa kigezo kuwa haikuwa imefikia ubora uliohitajika na uongozi wa lebo hiyo. Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba amechoshwa manyanyaso ambayo ameyapitia chini Label hiyo kwa muda miaka mitatu sasa huku akitishia kuichukulia Ziiki hatua kali za kisheria ili dunia ione udhalimu wake. Hata hivyo amemalizia kwa kusema iwapo lebo hiyo ingekubali wamaliza tofauti zao nyuma pazia hangeanika malalamiko yake kwenye mitandao ya kijamii lakini kutokana na ujeuri wao ameamua kuweka wazi ghadhabu zake.

Read More
 Avril na Tanasha Donna wasikitishwa na kampuni ya ZUKU kukatiza huduma za mtandao bila ilani

Avril na Tanasha Donna wasikitishwa na kampuni ya ZUKU kukatiza huduma za mtandao bila ilani

Wasanii Avril na Tanasha Donna wameonesha ghadhabu zao kwa kampuni ya Zuku kutokana na huduma duni ya mtandao. Kupitia mitandao yao ya kijamii wasanii hao wawili wametoa malalamiko yao kwa kampuni hiyo kufuatia kukosa huduma ya mtandao kwa kipindi cha siku tatu mfululizo. Hata hivyo wameichana kampuni ya Zuku kwa hatua ya kuwa na wahudumu wasiowajibikia majukumu ya kujibu simu za wateja wao wakati wa dharura huku wakitshia kuhamia makampuni mengine ambayo yanatoa huduma ya mtandao.

Read More
 Tanasha Donna akutana na mwanamasumbwi maarufu Duniani Floyd Mayweather.

Tanasha Donna akutana na mwanamasumbwi maarufu Duniani Floyd Mayweather.

Staa wa muziki nchini, Tanasha Donna ambaye kwa sasa yupo Dubai, akiwa mjini humo amekutana na mwanamasumbwi maarufu Duniani toka nchini Marekani Floyd Mayweather. Tanasha Donna ambaye yupo Dubai kwa shughuli zake za kimuziki, amekutana na Mayweather ambaye alitua jijini humo kwa ajili ya pambano lake na Deji ndani ya Cocacola Arena mwishoni mwa wikiendi iliyoisha. Donna ame share picha pamoja na video akiwa na mwanamasumbwi huyo kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram.

Read More
 Tanasha ataka watu kufanya dua kwa ajili ya maandamano na kinachoendelea Iran

Tanasha ataka watu kufanya dua kwa ajili ya maandamano na kinachoendelea Iran

Msanii kutoka Kenya Tanasha Donna amesikitishwa na taarifa ya uongo ambayo inasambaa mtandaoni kuwa Iran imetoa hukumu ya kifo kwa takriban watu 15,000 walioandamana kufuatia kifo cha Mahza Amini, binti aliyefarikiwa mikononi mwa polisi. Kupitia video yake aliyoichapisha kwenye mtandao wa Instagram Tanasha amewataka watu kufanya dua kwa ajili ya maandamano na kinachoendelea Iran badala ya kueneza propaganda kuwa wafungwa wanawake mabikra wanabakwa kwanza kabla ya hukumu ya kifo kutolewa kwao. Kauli yake imekuja mara baada ya Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau kupata ukosoaji mkubwa kutoka kwa serikali ya Iran mara baada ya kutumia mitandao yake ya kijamii kusema kwamba taifa hilo lilitoa hukumu ya kifo kwa watu 15,000 walioandamana kufuatia kifo cha Mahza Amini, aliyefarikiwa akiwa anashikiliwa na polisi kwa kosa la kutovalia vazi la Hijab.

Read More
 TANASHA AKANUSHA MADAI YA KUWAKIMBIA WAANDISHI WA HABARI

TANASHA AKANUSHA MADAI YA KUWAKIMBIA WAANDISHI WA HABARI

Msanii Tanasha Donna amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa ameanza kuwafungia vioo waandishi wa habari wanaotaka kufanya naye mahojiano kuhusu shughuli zake za kimuziki. Katika mahojiano na Mpasho, Tanasha amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwani watu walitafsiri vibaya kauli yake aliyotoa juzi kati kuhusu wanablogu wa Tanzania waliomchafulia jina kwa stori za kutunga. Mrembo huyo amesema yuko tayari kufanya mahojiano na mwaandishi yeyote wa habari ambaye ana nia njema ya kumuunga mkono kwenye harakati za kutanua wigo wa muziki wake uweze kuwafikia wengi. Katika hatua nyingine mrembo huyo amefunguka na kudai sababu kubwa ya yeye kubadilisha aina ya uimbaji katika muziki ni kutaka kukimbizana na kizazi cha sasa na sio kubakia pale alivyokuwa awali. Tanasha amedai suala la kubadilika ni jambo la kawaida huku akidai kuwa anachofanya kwa sasa ni kutaka kuendana na nyakati zilizopo kwani kuwa kwenye kiwanda cha muziki ambacho kina ushindani kuna hitaji msaani kuwa na ubunifu. Tanasha Donna kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake uitwao “Karma” ambao ameufanya kwa mahadhi ya muziki wa trap.

Read More
 TANASHA DONNA AWACHANA WANA BLOGU WA TANZANIA

TANASHA DONNA AWACHANA WANA BLOGU WA TANZANIA

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna amechukizwa na Mablogger wanaotumia maudhui yenye utata kutoka kwa wasanii kuuza maudhui yao. Kupitia Insta Story Tanasha amesema kuna Blogger toka Tanzania alimuomba kufanya naye mahojiano ambapo walizungumza kuhusu muziki na sanaa lakini mwisho wa siku kaenda kuandika vitu sivyo!. “Baadhi ya Wanablog hawana heshima, Blogger wa Kitanzania alinitumia ujumbe na alikuwa akiniita katika mahojiano. Niliwapa muda wangu ili wasijisikie nina kiburi kwani wamekuwa wakijaribu kunitafuta kwa muda sasa,” alisema Tanasha. Aliendelea kwa kusema kusema “Alinitumia maswali na kufanya ionekane kana kwamba analenga sanaa, hata kuulizwa kuhusu filamu mpya niliyoshirikishwa, kisha kuhaririwa na kuachwa sehemu ambayo itaonekana yenye utata zaidi”.

Read More
 TANASHA DONNA AWAJIA JUU WAANDAJI WA TUZO ZA KIMATAIFA

TANASHA DONNA AWAJIA JUU WAANDAJI WA TUZO ZA KIMATAIFA

Msanii wa kike nchini Tanasha Donna ameamua kuanika siri za tuzo za kimataifa akidai ni za kupangwa. Kupitia mfululizo ya posti zake kwenye mtandao wa Instagram (Instastory) amezituhumu tuzo hizo ambazo hajazitaja jina kuwa waliwahi kumpigia simu na kumtaka atoe hongo ili wamtangaze mshindi na alipokataa hakupewa tuzo. Tanasha ambaye anafanya vizuri na single yake mpya “Karma” amewataka waandaji wa tuzo kuacha kumteua kwenye vinyang’anyiro vya tuzo hizo. Hata hivyo hajabainika ni kitu gani kilimpelekea mrembo huyo kuibua tuhuma hizo dhidi ya tuzo za muziki.

Read More
 TANASHA DONNA ATHIBITISHA KUACHANA NA MPENZI WAKE MZUNGU

TANASHA DONNA ATHIBITISHA KUACHANA NA MPENZI WAKE MZUNGU

Msanii Tanasha Donna hatimaye amethibitisha kuwa yeye na mpenzi wake aliyekuwa akisemekana ni Mzungu wameachana. Kupitia Instagram live Tanasha amedai kuwa sababu ya kuachana kwao ni Usaliti ambapo amesema alichukizwa na kitendo cha mpenzi wake huyo kutoka kimapenzi na mwanamitindo mmoja barani ulaya licha ya kumueleza kuwa yupo single. Tanasha donna ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya “Karma” amesema hatompa nafasi nyingine jamaa huyo kwenye maisha yake kwa kuwa hapendi kabisa watu waongo.

Read More
 TANASHA DONNA AFICHUA KUWA MTOTO WAKE HAJAWAHI KUTANA NA MAMA YAKE MZAZI

TANASHA DONNA AFICHUA KUWA MTOTO WAKE HAJAWAHI KUTANA NA MAMA YAKE MZAZI

Msanii Tanasha Donna amefunguka tusiyoyajua kuhusu mtoto wake Naseeb Junior ambaye alizaa na staa wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz. Kupitia instagram live Tanasha amesema tangu mtoto wake huyo azaliwe hajawahi kumtambulisha kwa mama yake mzazi Diana Oketch. Tanasha ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya “Maradonna” amesema kumkutanisha mtoto wake Naseeb Junior na mama yake mzazi katika kipindi cha wiki tatu ijayo. Hata hivyo jambo hilo limezua hisia mseto miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wengi wakihoji kuwa inakuaje hajawahi mkutambulisha mtoto wake kwa mama yake mzazi licha ya kuwa amekuwa akisisitiza kwamba ana ukaribu na mama yake huyo. Utakumbuka tanasha juzi kati amekuwa vacation nchini dubai ambako alienda kwa ajili ya kazi zake za muziki lakini pia kusherekea birthday ya mtoto wake.

Read More