
Msanii wa muziki nchini Tanasha Donna ametangaza ujio wa ngoma yake mpya baada ya kimya cha muda mrefu bila kutoa hitsong yeyote.
Tanasha ameweka wazi taarifa hiyo kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea wimbo wake mpya ambao ameutaja utatoka rasmi wiki ijayo.
Mrembo huyo ambaye anaenda kuachia EP yake mpya baadae mwaka huu, kwa nyakati tofauti kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amekuwa akidokeza juu ya ujio wake mpya.
Ikumbukwe, ngoma yake ya mwisho kuitoa ilikuwa ni “Mood” ambayo ilitoka miezi 6 iliyopita na mpaka sasa ina zaidi ya views laki 4 kwenye mtandao wa Youtube.