
Msanii Tanasha Donna amefunguka tusiyoyajua kuhusu mtoto wake Naseeb Junior ambaye alizaa na staa wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz.
Kupitia instagram live Tanasha amesema tangu mtoto wake huyo azaliwe hajawahi kumtambulisha kwa mama yake mzazi Diana Oketch.
Tanasha ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya “Maradonna” amesema kumkutanisha mtoto wake Naseeb Junior na mama yake mzazi katika kipindi cha wiki tatu ijayo.
Hata hivyo jambo hilo limezua hisia mseto miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wengi wakihoji kuwa inakuaje hajawahi mkutambulisha mtoto wake kwa mama yake mzazi licha ya kuwa amekuwa akisisitiza kwamba ana ukaribu na mama yake huyo.
Utakumbuka tanasha juzi kati amekuwa vacation nchini dubai ambako alienda kwa ajili ya kazi zake za muziki lakini pia kusherekea birthday ya mtoto wake.