
Mwanamuziki wa kike kutoka nchini Nigeria Tems amekumbuka kipindi ambacho aliwekwa gerezani mwishoni mwa mwaka 2020 nchini Uganda.
Kupitia akaunti yake ya Twitter Terms ameandika “ Nyakati kama hizi mwaka jana nilikua gerezani na watoto na kina mama nchini Uganda. Sitaki kuamini vitu nilivyo viona”
Ikumbukwe Terms pamoja na mwanamuziki omahlay walitiwa mbaroni nchini Uganda baada ya kukiuka masharti ya COVID-19 na kufanya onyesho ambalo lilipelekea wawili hao kupelekwa gerezani