
Mwanamuziki nyota kutoka Nigeria, Tems, amezindua rasmi programu mpya ya kuwawezesha wanawake vijana kwenye tasnia ya muziki, iitwayo The Leading Vibe Initiative. Programu hiyo inalenga kuwapatia wanawake mafunzo na nyenzo muhimu za kufanikisha kazi zao katika sekta ya muziki.
Warsha ya kwanza chini ya mpango huu imepangwa kufanyika kwa siku mbili, kuanzia Agosti 8 hadi 9 jijini Lagos, Nigeria, ambapo washiriki watajifunza kuhusu uandishi wa nyimbo, uzalishaji wa muziki, pamoja na kushiriki midahalo na wataalam wa muziki. Pia kutakuwa na vikao vya studio kwa ajili ya kukuza ubunifu wa washiriki.
Mpango huu unawalenga wanawake 15 hadi 20 wenye nia na vipaji katika muziki, huku tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ikiwa Julai 13. Washiriki watapewa vifaa vya kisasa vya uzalishaji na rasilimali nyingine muhimu zitakazowawezesha kuendeleza kazi zao kwa ufanisi.
Tems amesema kuwa kupitia The Leading Vibe Initiative, anataka kuhakikisha kuwa wanawake barani Afrika wanapata nafasi ya kujiamini, kupata maarifa sahihi, na kuchangia katika maendeleo ya muziki ndani na nje ya bara.
“Ni wakati wa wanawake kuwa sauti kubwa katika muziki wa Afrika. Ninaamini wakipewa nafasi na zana sahihi, wanaweza kuvuka mipaka,” alisema Tems.
Tems, ambaye tayari ameweka historia kwa kushinda tuzo mbili za Grammy na kushika nafasi za juu kwenye chati za Billboard, anatarajia kupanua programu hii hadi miji mingine barani Afrika katika siku za uso