Entertainment

THE WEEKND ADOKEZA MPANGO WA KUBADILI JINA LA USANII

THE WEEKND ADOKEZA MPANGO WA KUBADILI JINA LA USANII

Mwanamuziki The Weeknd anafikiria kubadilisha jina lake la muziki na kutumia ‘Abel’ ambalo ni jina lake la kuzaliwa.

The Weeknd amefunguka matamanio yake hayo kupitia ukurasa wa Twitter, huku akihamasishwa na Kanye West ambaye alibadili jina lake na kuwa YE.

Mastaa kadhaa na mashabiki wa mkali huyo wameonesha kuunga mkono wazo hilo akiwemo mwimbaji John Legend.

The Weeknd ambaye anafahamika kama Abel Makkonen Tesfaye alizaliwa Toronto Canada mwaka 1990.

Wazazi wake ni raia wa Ethiopia ambao walikimbilia nchini Canada miaka ya 80.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *