Tiktoker kutoka Kenya, Kabuda, anayejulikana kwa maudhui yake ya kula chakula kingi mitandaoni, amezua gumzo baada ya kumtambulisha rasmi mpenzi wake kwa umma.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Kabuda ameposti video akiwa na mpenzi wake kwa jina la Gift Nasimiyu na kueleza kuwa anaingia mwaka wa 2026 akiwa na msichana yuleyule aliyekutana naye mwaka 2025, akisema wao kama couple mpya mjini.
Kwenye video hiyo, Kabuda ameonekana akiwa na furaha huku akijiamini zaidi na uamuzi wake wa kuweka wazi maisha yake ya mapenzi kwa umma.
Kilichoibua gumzo zaidi ni muonekano wa Gift Nasimiyu, ambaye ni mwembamba na mwenye umbo tofauti kabisa na Kabuda, ambaye anajulikana kwa unene wake uliopitiliza. Tofauti hiyo ya maumbile imeibua mjadala mpana, baadhi wakishangaa huku wengine wakisisitiza kuwa mapenzi hayapimwi kwa muonekano wa nje.