Entertainment

Dudu Baya Amwonya Mwijaku Kutoingilia Ugomvi wake na Mkubwa Fella

Dudu Baya Amwonya Mwijaku Kutoingilia Ugomvi wake na Mkubwa Fella

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Dudu Baya, amempa onyo kali mdau wa burudani, Mwijaku, akimtaka ajiondoe mara moja katika kile alichokiita vita ya mapinduzi kati yake na meneja Mkubwa Fella ambaye kwa sasa ni mgonjwa.

Akipiga stori na Bongo 24, Dudu amesema Mwijaku anatafuta kiki kwa kuingilia mjadala usiomuhusu, na akasisitiza kuwa akizidi kuingilia ugomvi huo, ataambulia kichapo cha mbwa msikitini

Kwa mujibu wa Dudu Baya, wanaopaswa kujibu hoja zinazomhusu Mkubwa Fella ni wasanii wakongwe waliopitia mikononi mwa meneja huyo, na siyo mtoto mdogo kama Mwijaku.

Amesema ukimya wa wasanii wakongwe unatokana na ukweli kwamba wengi wao wanafahamu tabia za ukatili na unyanyasaji walizofanyiwa na Mkubwa Fella, ikiwemo kuzimwa kwa vipaji na nyota za wasanii kadhaa.

Dudu ameongeza kuwa yuko tayari kuweka wazi maovu anayodai kufanywa na Mkubwa Fella ili jamii ya Watanzania ijue ukweli, akisema muda umefika wa ukweli kuanikwa bila woga.

Kauli hiyo ya Dudu Baya imekuja kufuatia Mwijaku kumtaka aonyeshe utu na heshima kwa Mkubwa Fella, hasa ikizingatiwa kuwa meneja huyo anaumwa. Mwijaku alimkosoa Dudu Baya baada ya kauli yake ya awali kwamba endapo Mkubwa Fella atafariki, hatofika kwenye mazishi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *