TikToker kutoka Kenya, Mjaka Mfine, amekiri kuchoshwa na maisha ya upweke, hatua iliyomfanya kutangaza rasmi kuanza mchakato wa kumtafuta mwanaume rijali atakayempa mapenzi ya dhati.
Kupitia video inayotembea mtandaoni, Mrembo huyo amesema yuko tayari kuingia kwenye uhusiano wa kweli na anahitaji mwanaume atakayemhudumia, kumjali na kumuonyesha upendo wa dhati bila maigizo. Ameeleza kuwa kwa sasa anatafuta mapenzi yenye heshima, uaminifu na uthabiti, tofauti na mahusiano ya kuonekana mitandaoni.
Mjaka Mfine amesisitiza kuwa anataka mwanaume anayejua wajibu wake, mwenye uwezo wa kusimama kama mwanaume kamili na aliye tayari kumpa usalama wa kihisia pamoja na mapenzi ya kweli.
Kauli hiyo imekuja katika kipindi ambacho Mjaka Mfine amekuwa akihusishwa na content creator mwenzake Mokaya, kutokana na ukaribu wao mkubwa ambao umeibua maswali mengi miongoni mwa mashabiki. Hata hivyo, bado haijabainika iwapo ukaribu huo ni wa kikazi au unaashiria uwepo wa uhusiano wa kimapenzi.