Sports news

Timu Ya Hoki Ya Wanawake Ya Kenya Yapokea Udhamini Kutimiza Ndoto Ya Olimpiki

Timu Ya Hoki Ya Wanawake Ya Kenya Yapokea Udhamini Kutimiza Ndoto Ya Olimpiki

Matumaini ya Kenya ya kushirikisha timu ya hoki kwenye michezo ya Olimpiki mwaka 2028 jijini Los Angeles yamepigwa jeki baada ya kamati ya Olimpiki humu nchini kuzindua ufadhili kutoka kwa kamati ya Olimpiki duniani kwa timu ya wanawake ya hoki.

Timu hiyo ya wanawake ya hoki sasa inatarajiwa kuanza mpango wa maandalizi wa kufuzu kwa michezo hiyo ya Olimpiki.

Ufadhili huo unajiri baada ya timu ya wanawake ya hoki kuandikisha matokeo bora kwenye mashindano ya bara Afrika, ilipomaliza ya tatu na hivyo kuchupa katika orodha ya hoki ya bara Afrika, na pia kujiongezea matumaini ya kuandikisha matokeo bora katika michuano ijayo ya kufuzu kwa mashindano ya kimataifa.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, kinara wa NOC-K Shadrack Maluki alitangaza kuwa, timu hiyo imepokea udhamini wa dola elfu 50 za marekani kwenye mpango huo ambazo zitatumiwa kusaidia katika mazoezi yake, maandalizi na pia kushiriki kwake katika mashindano ya kamatifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *