
Malkia wa muziki wa AfroBeats, Tiwa Savage, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kufichua vigezo anavyovitaka kwa mwanaume wa ndoto zake.
Akiwa kwenye mahojiano ya hivi karibuni, Tiwa alieleza kuwa hana mpenzi kwa sasa, na si kwa sababu kuna uhaba wa wanaume, bali ni kutokana na matarajio maalum aliyojiwekea.
Kwa sasa, anatafuta mwanaume mwenye ndege binafsi (private jet), mwenye boti, na asiye na changamoto au drama zinazohusiana na wanawake wengine. Anaamini huenda vigezo hivyo vikawa sababu ya kutompata mtu anayemfaa hadi sasa.
Kauli hiyo imezua mijadala mseto mitandaoni. Baadhi ya mashabiki wamepongeza msimamo wake kama ishara ya kujua thamani yake, huku wengine wakiona vigezo hivyo kuwa vya hali ya juu sana.
Tiwa Savage, ambaye ameweka alama kubwa kwenye muziki wa Afrika na kimataifa, anaendelea kuwa mfano wa mwanamke jasiri, mwenye malengo na maamuzi thabiti hata linapokuja suala la mapenzi.