Entertainment

Tom Daktari Awakosoa Wasanii Wanaotumia Kifo cha Raila Kutafuta Kiki

Tom Daktari Awakosoa Wasanii Wanaotumia Kifo cha Raila Kutafuta Kiki

Mchekeshaji wa Kenya, Tom Daktari, ameonyesha masikitiko yake kwa baadhi ya wasanii nchini humo wanaotumia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Amolo Odinga, kujitafutia umaarufu na kiki mitandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tom Daktari ameeleza kushangazwa na namna ambavyo baadhi ya wasanii wamegeuza maombolezo kuwa fursa ya kupata views kwenye YouTube kupitia nyimbo za kuomboleza.

Mchekeshaji huyo, amebainisha kuwa nyimbo za tribute hazipaswi kutumika kama njia ya kujitangaza au kupata umaarufu, bali ni ishara ya heshima na upendo kwa hayati Raila Odinga. Aidha, amewataka wasanii waelewe kuwa kuna mipaka kati ya sanaa na maadili ya kijamii, hasa katika nyakati za huzuni kama hizi.

Tom Daktari amewashauri wasanii hao kuwa na utu, kuheshimu hisia za Wakenya na familia ya Odinga badala ya kutumia maombolezo kama njia ya kujitafutia umaarufu. Amesema huu si wakati wa mashindano ya nani ana nyimbo nyingi au views nyingi, bali wa kuonyesha umoja, upendo na heshima kwa kiongozi aliyegusa maisha ya wengi.

Kauli yake inakuja saa chache baada ya msanii Bahati kujitangaza kuwa msanii namba moja Afrika Mashariki kufuatia wimbo wake “Bye Bye Baba” kupata zaidi ya views milioni moja ndani ya siku moja kwenye mtandao wa YouTube.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *