
Rapa kutoka nchini Canada Tory Lanez, amedaiwa kupitia nyakati ngumu sana kwenye maisha yake na anajutia kwanini hakukiri makosa yake Mahakamani mwezi Disemba.
Tovuti ya Rolling Stone imeandika taarifa hiyo wakati Tory Lanez akiwa rumande kwa sasa akisubiri hukumu yake ambayo itasomwa Februari 28 mwaka huu ambapo huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 22 na miezi 8 Jela.
Utakumbuka Tory Lanez alikutwa na hatia ya makosa matatu ikiwemo la kumshambulia na kumjeruhi kwa risasi aliyekuwa mpenzi wake mwanamuziki Megan Thee Stallion.