Entertainment

Tory Lanez Ajeruhiwa Vibaya Gerezani, Inadaiwa Alichomwa Visu Mara 14

Tory Lanez Ajeruhiwa Vibaya Gerezani, Inadaiwa Alichomwa Visu Mara 14

Msanii wa muziki kutoka Canada, Tory Lanez, anaripotiwa kujeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa gerezani, akidaiwa kuchomwa visu mara 14 na mtu anayedaiwa kuwa mwanachama wa genge hatari la kihuni kutoka Mexico.

Kwa mujibu wa sauti inayosambaa mitandaoni ya Wack 100, mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya burudani na anayejulikana kwa mara kwa mara kudai kuwa na taarifa za ndani, genge hilo la kihuni la Mexico linahusishwa na shambulio hilo la kushangaza lililotokea katika Gereza la North Kern, nchini Marekani.

Katika sauti hiyo, Wack 100 anasikika akisema:

 “Walimkamata Tory Lanez ndani. Nasikia alichomwa mara 14. Hili ni genge la kihuni kutoka upande wa Kusini mwa mpaka. Jamaa wana msimamo mkali, na wakimlenga mtu, si mchezo.”

Ingawa hakutaja jina la chanzo chake wala kutoa ushahidi wa moja kwa moja, Wack 100 alionya kuwa tukio hilo linaweza kuchochea mzozo mkubwa baina ya makundi ya kihalifu ndani ya gereza hilo. Hadi sasa, sababu rasmi ya shambulio hilo haijabainishwa, huku uchunguzi ukiendelea kufanywa na mamlaka husika.

Mamlaka za magereza zimethibitisha kwamba tukio la vurugu lilitokea katika gereza hilo na kwamba mmoja wa wafungwa alijeruhiwa vibaya. Hata hivyo, hawakutaja jina la Tory Lanez wala kueleza undani wa shambulio hilo kwa wakati huu. Vyanzo vya karibu na kesi hiyo vinaeleza kuwa huenda msanii huyo akahamishiwa kwenye gereza jingine kwa sababu za kiusalama.

Mashabiki wake pamoja na watu mashuhuri kwenye mitandao ya kijamii wameonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya Tory, wakisubiri tamko rasmi kutoka kwa mawakili wake au familia yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *