Entertainment

Tory Lanez amfuta kazi mwanasheria wake

Tory Lanez amfuta kazi mwanasheria wake

Mitandao mbalimbali ya nchini Marekani imeripoti kwamba Rapa Tory Lanez amemfukuza kazi Mwanasheria wake na kumuajiri David Kenner ambaye ana uzoefu mkubwa.

David Kenner anatajwa kuwawakilisha wasanii na watu maarufu kwenye Kesi zao kubwa ikiwemo ile ya Suge Knight, CEO wa zamani wa Label ya Death Row.

Lakini watalaamu wa masuala ya sheria wanasema, inaweza kuwa sio muda sahihi kwa Kenner kuweka mguu wake kwenye Kesi ya Tory Lanez kwani amechelewa sana, Kabla ya Mahakama kumkuta na hatia ndio ungekuwa

muda mzuri zaidi.

Tory Lanez ambaye yupo rumande kwa sasa, mahakama itatoa hukumu ya kesi yake Januari 27 mwaka huu hii ni baada ya kukutwa na hatia kumpiga risasi Megan Thee Stallion.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *