
Mwanamuziki Tory Lanez amewekwa Kifungo cha ndani (House Arrest) kufuatia sakata lake la kumshambulia August Alsina mapema mwezi uliopita.
Jaji amesema kwa kitendo kile, Tory Lanez ameharibu masharti ya dhamana kwenye shtaka lake dhidi ya Megan Thee Stallion.
Lanez atakuwa chini ya uangalizi wa kifungo cha ndani kutokana na sababu zilizotolewa na waendesha mashtaka kwamba amekuwa mtu hatari kwenye Jamii, na atakaa hadi pindi Kesi yake ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion ikianza kusikilizwa, November 28 mwaka huu.